Featured

    Featured Posts

KITUO KIKUU CHA MABASI CHA DODOMA KUZINDULIWA HIVI KARIBUNI, MKURUGENZI WA JIJI AFUNGUKA


Charles James, Michuzi TV

JIJI la Dodoma limesema ifikapo Juni 30 mwaka huu ndio itakua mwisho kwa Mabasi makubwa ya abiria kupaki nje ya Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi katika mkutano wake na wandishi wa habari wakati alipotembelea Ujenzi wa Kituo hicho kinachojengwa katika eneo la Nzuguni.

Kunambi amesema ujenzi wa Kituo hiko ambacho kitakua kikubwa kuliko vyote kwa ukanda wa Afrika Mashariki tayari umekamilika na muda wowote kuanzia sasa wananchi watatangaziwa tarehe ya kuanza kutumika.

Amewataka wamiliki wa Mabasi wote kuhakikisha mabasi yao yanapaki katika Kituo hiko na ambaye atalaza nje ya hapo ni lazima awe na eneo lake maalum (yard) ambayo Jiji la Dodoma itakua imeipitisha.

" Kukamilika kwa ujenzi huu kunaenda kuipa hadhi Jiji la Dodoma ambalo ndio Makao Makuu ya Nchi na Serikali, hivyo hatuna muda kumshukuru Rais Magufuli ambaye yeye ndiye hasa amechangia kupatikana kwa kituo hiki.

Uwepo wa Kituo hiki kutainufaisha Halmashauri yetu kimapato na pia kuinua maisha ya wananchi wetu ambao wengi wao wameomba nafasi ya kuwekeza biashara zao ndani ya kituo hiki na tayari wenye sifa wameshapatikana na kuanzia kesho tutaweka majina yao hadharani kwenye ubao wa Jiji na kwenye mitandao," Amesema Kunambi.

Amesema Kituo hiko kina hadhi ya kimataifa ndio maana kina eneo maalum la VIP ambalo wasafiri wanaweza kusubiri Mabasi yao wakiwa hapo wakiangalia televisheni, kula na kunywa kupitia migahawa ya kisasa iliyopo lakini pia kupumzika.
 Muonekano wa mbele wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Dodoma ambacho kinatajwa kuwa kikubwa na cha kisasa Afrika Mashariki.
 Sehemu ya ndani ya Kituo Kikuu cha Mabasi cha Dodoma inavyoonekana baada ya kukamilika
 Eneo la VIP katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Dodoma ambalo lina Mgahawa na Bar kama ambavyo linaonekana
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi akizungumza na wandishi wa habari leo katika eneo la Kituo Kikuu cha Mabasi ambacho kinatarajiwa kuanza kazi hivi karibuni.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana