Na Amiri kilagalila,Njombe
Changamoto ya usafiri ili kuwafikia wananchi katika vijiji mbalimbali kwa maofisa tarafa mkoani Njombe sasa imepatiwa ufumbuzi baada ya serikali kugawa Pikipiki kwa kila ofisa hatua itakayochochea uhamasishaji shughuli za maendeleo.
Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa pikipiki na katibu tawala mkoa wa Njombe kwa niaba ya mkuu wa mkoa baadhi ya maofisa tarafa akiwemo Lilian Nyemele na Damas Kavindi wanasema tatizo la usafiri kwao limekuwa gumu ili kuwafikia wananchi hasa huko vijijini na kwamba sasa changamoto hiyo itapungua baada ya Rais magufuli kuwakumbuka.
“Hiki ni kipindi cha mavuno kwa hiyo nitafuatilia kwa karibu sana kwasababu kitendea kazi ninacho,vile vile kitanisaidia kwenda kuendelea kuhamasisha wananchi katika kutoa elimu dhidi ya mapambano ya ugonjwa huu wa covid-19”alisema Lilian Nyemele
Akikabidhi pikipiki hizo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe katibu tawala wa mkoa Catalina Revocati anatumia fursa hiyo kuhakikisha wanakwenda kutekeleza majukumu yao kwa weledi kwa kutumia vyombo hivyo.
“Mkoa wa Njombe umepokea Piki piki 18 ambazo zinatosha tarafa zote za mkoa huu,lengo kubwa ni kuhakikisha maafisa tarafa wanatekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa”alisema Catalina Revocati
Emmanuel George ni katibu tawala wilaya ya Njombe na Edward Manga ni katibu tawala wilaya ya Wanging'ombe ambao wanakiri kuzipokea pikipiki hizo kwa niaba ya maofisa tarafa na kuahidi kuzitumia kama walivyopewa maelekezo.
“Lakini pia tunaahidi hivi vyombo tutavitunza ili vikafanye ile kazi inayolengwa na shukrani kubwa zimuendee Rais kwa kuhakikisha maafisa hawa wanapata usafiri” alisema Emmanuel George Kwa upande wake mwenyekiti wa maofisa tarafa hao mkoa mzee Linus Malamba anasema pamoja na kuahidi kuzitunza pikipiki hizo lakini wanaomba kusaidiwa katika suala la mafuta na ukarabati.
Katibu tawala wa mkoa Catalina Revocati akizungumza kwa kifupi na maafisa tarafa mkoa wa Njombe kabla ya kuwakabidhi Piki piki kwa ajili usafiri kuyafikia maeneo yao ya kazi mapema.
Piki piki zilizotolewa na serikali kwa ajili ya maafisa tarafa wa mkoa wa Njombe,na kukabidhiwa siku ya leo katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Njombe.
Emmanuel George katibu tawala wilaya ya Njombe akitoa shukrani kwa Rais mara baada ya kukabidhiwa pikipiki kwa ajili ya maafisa tarafa wa wilaya ya Njombe.
Maafisa tarafa na makatibu tawala wa halmashauri za wilaya wakiwa makini kumsikiliza katibu tawala wa mkoa wa Njombe wakati wakikabidhiwa Piki Piki.
Post a Comment