Featured

    Featured Posts

MJUE RAIS MTEULE WA BURUNDI


Evariste Ndayishimiye pumping fist in the airHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEvariste Ndayishimiye ni mshirika wa karibu wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Ni matokekeao ambayo yalikuwa yanatarajiwa. Tume ya uchaguzi hii leo imemtangaza Meja Jenerali mstaafu Evariste Ndayishimiye kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika juma lililopita.
Evariste atachukua nafasi ya Rais Pierre Nkurunziza mbaye ameliongoza taifa hilo la Afrika Mashariki kwa miaka 15.
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza Ndayishimiye ni nani? mwanasiasa huyo ni mtu wa karibu wa Nkurunziza na amekuwa Katibu Mkuu wa Chama tawala CNDD-FDD tangu mwaka 2016.
Alizaliwa mwaka wa 1968 katika mkoa wa Gitega, eneo la kati mwa taifa hilo.

Uhusiano wa Ndayishimiye na CNDD-FDD

Bwana Ndayishimiye ni miongoni mwa waliokuwa waasi wa CNDD-FDD waliojiunga na kundi hilo baada ya kunusurika katika mauaji ya kikabila ya wanafunzi Wahutu katika chuo kikuu cha Burundi mwaka 1995, kufuatia mauaji ya rais Melchior Ndadaye mnamo mwaka wa 1993.
Baadae kundi la CNDD-FDD lilibadilishwa na kuwa chama cha kisiasa ambacho kilianza kushiriki katika mazungmzo ya amani mjini Arusha Tanzania mwaka wa 2000 na kuafikiana kuhusu usitishwaji wa vita.
Wakati kundi la waasi la CNDD-FDD lilipojiunga na serikali mwaka wa 2003, Ndayishimiye tayari alikuwa amepandishwa cheo cha Meja Jenerali, na alihamishwa aende kuhudumu katika makao makuu ya jeshi la taifa.
Jenerali NdayishimiyeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Ndayishimiye aliteuliwa waziri wa usalama wa ndani na usalama wa umma nchini Burundi baada ya rais Nkurunziza kushinda uchaguzi mkuu wa 2005, na badaye kuhamishwa hadi ofisi ya rais mwaka 2007 ambapo alihudumu kama mshauri wa kijeshi.

Msimamo wa kadri

Wachanganuzi wa siasa za Burundi wanasema kwamba Jenerali Ndayishimiye ni mtu mwenye msimamo wa kadri asiyekimbilia mambo.
Wakati wa mzozo uliokumba Burundi mwaka wa 2015 kufuatia jaribio la mapinduzi, jenerali Ndayishimiye ni miongoni mwa viongozi wachache waandamizi jeshini ambao hawakutajwa katika orodha ya wale waliohusika katika uhalifu dhidi ya binadamu na mashirika ya kimataifa.
Kuna wale ambao pia wanasema Jenerali Ndayishimiye hatabiriki katika misimamo yake.
Mdadisi wa kisiasa na mwandishi wa vitabu nchini Burundi David Gakunzi anasema tabia ya kutotabirika huenda ikawashawishi wapinzani kumuunga mkono shingo upande.
"Kwa mfano, Ndayishimiye mwanzo alipinga uamuzi wa Rais Nkurunziza wa kutaka kugombea urais kwa muhula wa tatu mwaka wa 2015 ingawa badaye alibadilisha nia na kumuunga mkono" anasema Gakunzi.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana