Featured

    Featured Posts

MTATURU ASEMA UCHAGUZI WA 2020 VUMBI LA USHINDI KWA CCM LITATIMKA.

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu (pichani) amesema katika uchaguzi mkuu wa Octoba mwaka huu vumbi la ushindi Kwa Chama Cha Mapinduzi(CCM) litatimka kutokana na utendaji mzuri wa Rais Dkt John Magufuli.
Mtaturu amesema hayo Mei 15 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia bajeti ya wizara ya Fedha na mipango.
“Ukiangalia vyama vingine ni kama vikundi vya kutafuta maslahi yao binafsi,lakini CCM tangu Uhuru tumeendelea kuongoza nchi hii na kwa hakika tutaona vumbi litakavyotimka katika uchaguzi,na CCM itashinda kwa kishindo,”alisema Mtaturu.
Amesema kutokana na utendaji wake mzuri  watanzania wamemuelewa na aliyoyafanya na kamwe hayatafutika kwenye uso wa watanzania.
“Nimtie moyo Rais Dkt John Magufuli,kwa hakika watanzania wamemuelewa na hawatamuacha,yote aliyoyafanya hayatafutika katika uso wa watanzania,nimtakie kila la kheri,sisi wapiganaji tupo pamoja nay eye,na kwa Singida Mashariki nimuhakikishie kura nyingi,mbunge nipo na madiwani wote watapatikana wa CCM,”alisema Mtaturu.
Akizungumzia kuhusu wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)walioacha kuhudhuria vikao vya bunge kwa madai ya kujiweka karantini ili kujikinga na virusi vya Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu(COVID 19)amesema watanzania waendelee kuchapa kazi Kama ambavyo Rais Magufuli amekuwa akisisitiza maana ugonjwa huo haujulikani utaisha lini.
“Covid 19 tunaambiwa ipo na tutaendelea kuishi nayo,tumeona waziri ameeleza namna anavyojipanga,naomba tuendelee kujipanga ndio maana Rais Magufuli ameonyeshwa maono na Mungu kuwa hatuwezi kuwa lockdown ambayo hatuju itaisha lini,Mungu mbariki sana,
Amesema wao kama wabunge wa CCM waliochaguliwa na waanchi wataendelea kusimama na waanchi maana pamoja na uwepo wa ugonjwa huo lakini lazima maisha yaendelee na kutoa pole kwa wote walioathirika na uwepo wa virusi hivyo.
“Leo tunaona kuna wenzetu waliacha kuja bunge na kujiweka karantini,sasa wamemaliza karantini wameanza kujitokeza humu,lakini ukiwauliza je uwoga wenu wa Corona umeishia wapi hawawezi kukupa jibu la kawaida,niwaombe watanzania waone aina ya watu ambao hawana dhamira ya kuleta maendeleo,

“Unapokuwa na aina ya vyama vya siasa ni lazima uwe na vyama vyenye focus ya kuwatumikia wananchi,na mnaona wenyewe watanzania wameona vyama hivi kuna baadhi ya vyama tukikutana octoba kitatoka kuwa chama cha siasa kitakuwa ni kikudi cha watu wawili watatu,”aliongeza Mtaturu.
AIOMBA SERIKALI KUTUPIA JICHO WASTAFU.
Mtaturu ameiomba serikali kuwalipa mapema wastaafu mafao yao ambao wamelitumikia Taifa hili kwa uadilifu.
 “Katika wilaya ya Ikungi kuna wazee wawili Mohammed Ntandu na Gamiliel Massawe wanalalamika hawajatendewa haki yao mpaka sasa hivi miezi saba ,wakienda  kwa wenzetu NSSF hawawapi majibu mazuri naomba mh waziri kuwe nzuri kati ya mikoa na makao makuu hazina ili kuwasaidia wastaafu wapate mafao yao mapema,”alisema Mtaturu.
Mbali na hilo ameiomba Wizara itoe fedha kwa ajili ya mradi wa umwagiliaji wa Mang’onyi  Kata ya Makiungu kwa kuwa mradi huo una faida nyingi kwa wananchi,lakini kwa halmashauri pia.
“Kuna mradi wa skimu ya umwagiliaji ya Mang’onyi,hiyo skimu ilitengewa  fedha mwaka 2017/2018 ilitengewa shilingi milioni 100 lakini fedha zile hazikwenda leo hii lile bwawa kina chake kimepungua hivyo hatuwezi kuwa na maji ya kutosha na mwaka huu mvua  zilivyokuwa nyingi lile bwawa lilitapika na kutaka kuleta athari  kwa wananchi.
“Naomba fedha tunazoomba tuwe tunapewa ili tuweze kuboresha ile skimu ambayo ipo pale itaenda kunufaisha wakulima wengi,”alisema.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana