Mmoja wa wanamuziki mahiri nchini na mwenye sauti yenye mvuto, Mabrouk Hamis Omar, maarufu Babu Njenje(pichani), ametangulia mbele ya haki.
Babu Njenje amefariki leo alfajiri baada ya kuugua kwa muda mrefu. Alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kupooza mwili.
Hadi mauti yalipomchukua, Babu Njenje alikuwa mwimbaji wa bendi ya The Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa John Kitime, ambaye ni mmoja wa wanamuziki wa kundi hilo, msiba upo mtaa wa Mindu, Upanga, ambako Babu Njenje alikuwa akiishi.
Babu Njenje atakumbukwa kwa nyimbo zake nyingi zikiwemo Njenje, Kinyaunyau na nyingine nyingi.
Hakika sisi sote ni waja wa Allah kwake tutarejea
Post a Comment