Ikulu, Chato
Rais Dk. John Magufuli amemrejesha kwenye Baraza lake la Mawaziri Mbunge wa Iramba Magharibi Dk. Mwigulu Lameck Nchemba (Pichani) kwa kumteua kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Taarifa iliyotolewa jioni hii na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, imesema uteuzi wa Dk. Mwigulu Lameck Nchemba unaanza leo tarehe 02 Mei, 2020.
"Dk. Mwigulu Lameck Nchemba anachukua nafasi ya Balozi Dk. Augustine Philip Mahiga aliyefariki dunia jana tarehe 01 Mei, 2020", imesema taarifa hiyo.
Post a Comment