Na Lydia Lugakila
KAGERA
Wananchi Mkoani Kagera wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kutoa taarifa zisizo za kweli kwa kutumia namba ya tahadhali inayotumika kutoa taarifa kwa jeshi la zimamoto na uokoaji.
kauli hiyo imetolewa na mkaguzi wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Kagera Thomas Majuto wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ambapo amesema kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia vibaya namba ya tahadhali inatumika kutoa taarifa za majanga yakiwemo ya moto.
Aidha katika hatua nyingine Majuto amewahimiza watumiaji wa gesi kuhakikisha wanajenga uratibu wa kukagua mapaipu ya majiko ya gesi ili kuepuka majanga ya moto.
Hata hivyo Mkaguzi huyo ametoa wito kwa madreva wa vyombo vya moto kuacha tabia ya kupakia mafuta katika vituo vya mafuta wakiwa wamebeba abiria katika vyombo vyao vya moto jambo ambalo ni hatari .
Post a Comment