Featured

    Featured Posts

VURUGU ZAZUKA MAREKANI BAADA YA MTU MWEUSI GEORGE FLOYD KUFARIKI MIKONONI MWA POLISI


Waanndamanaji walifika kwenye eneo ambalo polisi wanaohusika na mauaji wanadhaniwa kufanya kaziHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWaanndamanaji walifika kwenye eneo ambalo polisi wanaohusika na mauaji wanadhaniwa kufanya kazi
Kumekuwa na vurugu na mapambano kati ya polisi na waandamanaji katika mji wa Minneapolis nchini Marekani baada ya kifo cha mwanaume mmoja mweusi akiwa mikononi mwa polisi
Polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi na waandamanaji walirusha mawe na kupulizia mapambo ya graffiti kwenye magari ya polisi.
Kilichotokea kwenye maandamano
Walianza siku ya Jumanne jioni, wakati mamia ya watu walipofika katika eneo ambalo tukio lilitokea, Jumatatu jioni.
Waratibu walijaribu kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani na kuzingatia masharti ya kukaa mbalimbali, waandamanaji waliimga ''siwezi kupumua,'' na ''ingeweza kuwa mimi''.
Bango lililoandikwa jina la mwanaume aliyeuawaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBango lililoandikwa jina la mwanaume aliyeuawa
Mmoja wa waandamanaji Anitha Murray aliliambia gazeti la Washinton Post: ''inaogopesha kuwa hapa wakati wa janga la corona, lakini kwa nini nijiweke mbali?''
Kundi la mamia ya watu baadae waliandamana mpaka kwenye idara ya polisi 3rd Precinct, ambapo maafisa waliohusika na kifo hicho walikuwa wakifanya kazi.
Mtu mmoja alikiambia chombo cha habari cha CBS: ''Hii ni mbaya sana. Polisi lazima watambue kuwa hali hii wameitengeneza wenyewe.''
Polisi wamesema kuwa mtu mmoja amejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi lakini taarifa za kina hazijatolewa kuhusu tukio hilo.
Video ya tukio hilo la Minneapolis iliwekwa kwenye mtandao wa kijamiiHaki miliki ya pichaDARNELLA FRAZIER
Image captionVideo ya tukio hilo la Minneapolis iliwekwa kwenye mtandao wa kijamii
Maafisa wanne wa polisi katika jimbo la Minnesota nchini Marekani wamefutwa kazi kufuatia kifo cha mtu mweusi ambaye alikuwa amekamatwa na kuonekana akizuiliwa chini kwa kushikwa shingo.
Afisa mkuu wa polisi katika jimbo hilo Medaria Arradondo amesema kwamba maafisa hao wanne sasa ''sio wafanyakzi wa kikosi hicho''.
Kanda ya video inaonesha, mtu huyo kwa jina George Floyd , akilia na kuwaambia maafisa hao weupe ''siwezi kupumua''.
Kisa hicho kinafanana na kile cha Eric Garner, mtu mweusi aliyefariki akikamatwa na polisi mjini New York mwaka 2014.
Shirika la ujasusi nchini Marekani FBi lilisema litachunguza kisa hicho cha Minneapolis kilichofanyika Jumatatu jioni.
George FloydHaki miliki ya pichaTWITTER/RUTH RICHARDSON
Image captionGeorge Floyd aliwaambia polisi mara kadhaa kwamba hawezi kupumua
Maafisa wa polisi wa Minnesota walisema kwamba Floyd mwenye umri wa miaka 46 , ambaye alikuwa anafanya kazi kama afisa wa usalama katika mkahawa mmoja alifariki akifanyiwa matibabu kufuatia malumbano na maafisa wa polisi.
Siku ya Jumanne, Meya Jacob Frey alithibitisha kwamba maafisa hao wanne waliohusishwa na kisa hicho wamefutwa kazi. ''Huu ndio uamuzi tuliochukua''.
Katika mkutano na vyombo vya habari mapema, bwana Frey alikitaja kisa hicho kama cha kushangaza.
''Ninaamini kwamba kile nilichokiona ni kitendo cha makosa kwa kiwango chochote kile'' , alisema.
''Kuwa mtu mweusi nchini Marekani hakustahili kuwa hukumu ya kifo''.
Ni madai ya hivi karubuni ya unyanyasaji unaotekelezwa na maafisa wa polisi dhidi ya Wamarekani weusi.
Visa maarufu vya hivi karibuni vinashirikisha afisa mmoja wa eneo la Maryland ambaye alimpiga risasi mtu mmoja akiwa ndani ya gari la kupiga doria.
Kisa hicho cha Minneapolis kilianza baada ya ripoti kwamba mteja mmoja alikuwa anajaribu kutumia noti bandia ya dola 20 katika duka moja.
Afisa huyo alimuona mshukiwa akiwa ndani ya gari lake, mtu huyo alikataa kukamatwa kulingana na maafisa wa polisi.
Waliambiwa kwamba mtu huyo ambaye hajatambulika alikuwa ameketi juu ya gari la rangi ya buluu na alionekana kana kwamba ametumia kishawishi fulani.
Waandamanaji wakimuombe George Floyd, ambaye kifo chake kimezua mjadala wa ukatili wa polisi MarekaniHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWaandamanaji wakimuombea George Floyd, ambaye kifo chake kimezua mjadala wa ukatili wa polisi Marekani
Baada ya kuagizwa kuondoka na kusimama kando ya gari hilo , jamaa huyo alikataa kukakamtwa lakini maafisa walifanikiwa kumfunga mikono yake kwa pingu na akaonekana kana kwamba alikuwa anaugua tatizo la tiba., taarifa hiyo iliongezea.
Katika kanda hiyo ya dakika 10 iliochukuliwa na shahidi , mtu huyo aliwekwa ardhini na afisa huyo na katika wakati mmoja alisikika akisema ''musiniue''.
Shahidi mmoja alisikika akimwambia afisa huyo kuondoa goti lake katika shingo ya mshukiwa huyo, akidai kwamba alikuwa hayumbi.
Mwengine alisema pua yake inatoka damu, huku mwengine akiomba ''ondoka katika shingo yake''.
Mtu huyo anaonekana ametulia kabla ya kuingizwa katika ambulansi na kuondoka naye.
Maafisa wa polisi wanasema kwamba hakuna silaha iliotumika wakati wa kisa hicho , na kwamba picha zimepelekwa katika shirika la ujasusi la kukabiliana na uhalifu la Minnesota, ambalo linachunguza kesi hiyo.
Siku ya Jumanne jioni maafisa walitumia vitoa machozi kutawanya maandamano ya umma nje ya kituo cha polisi mjini Mineapolis , kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilo.
Mwandishi mmoja wa gazeti la The Star Tribune alituma ujumbe wa twitter kwamba alikuwa amepigwa na risasi bandia iliofyatuliwa na polisi.
Ripota mmoja wa runinga ya KTSV alituma ujumbe wa Twitter akisema kwamba waandamanaji walivunja vioo katika kituo hicho na kuchora maandishi machafu katika gari moja la polisi.
Maafisa wa polisi walisema katika taarifa yao awali kuhusu kifo cha Geore Floyd: Baada ya kupata habari zaidi, imebainika kwamba shirika la ujasusi nchini Marekani FBI litashirika katika uchunguzi huo.
Akizungumza kwa vyombo vya habari vya Marekani siku ya Jumanne, Afisa mkuu Arradondo alisema kwamba sera za kikosi cha polisi kuhusu kumdhibiti mshukiwa zitachunguzwa kama mojawapo ya uchunguzi huo.
Kulingana na chombo cha habari cha AP, maafisa wa polisi wa Minneapolis wanaruhusiwa kupitia sera ya kutumia nguvu kuweka magoti yao katika shingo ya mshukiwa iwapo kitendo hicho hakitaathiri njia za kupumua za mshukiwa.
Alipoulizwa kuhusu uchunguzi huo wa FBI Arradondo alisema , aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kupokea habari zaidi kutoka chanzo kimoja cha kijamii.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana