Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewashambulia Wapalestina waliokuwa wamefika katika Msikiti wa Al-Aqsa mjini Quds kwa ajili ya Ibada.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, wanajeshi wa utawala ghasibu siku ya Jumapili asubuhi waliwashambulia Wapalestina waliokuwa wamefika kando kando ya msikiti wa Al Aqsa kwa ajili ya Swala ya siku kuu ya Eid el Fitri.
Pamoja na kuwepo utumiaji mabavu wa askari wa Kizayuni, Wapalestina hao hatimaye waliweza kuswali Swala siku kuu ya Eid el Fitri katika Medani ya Al Ghazala katika uwanja wa Msikiti wa Al Aqsa katika lango la Babul Asbaat la msikiti huo.
Eneo la ndani la Msikiti wa Al Aqsa limefungwa kwa muda wa miezi miwili sasa kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 na kwa mujibu wa Idara ya Wakfu ya Palestina, msikiti huo utafunguliwa kikamilifu baada ya siku kuu ya Eid el Fitri.
Leo Jumapili, tarehe Mosi Shawwal ni siku kuu ya Idul Fitr katika aghalabu ya nchi za dunia.
Post a Comment