Mwongozo huo umetolewa na Wizara hiyo kwa lengo la kuhakikisha makampuni hayo yanajiweka tayari ili kuwaepusha watalii kupata maambukizi ya Virusi hivyo na kusisitiza kuwa sehemu zote ambazo ni rahisi kuguswa na mtu yoyote, wahakikishe zinasafishwa kwa kutumia sanitizer zilizothibitishwa.
Aidha Wizara imesisitiza pia kila gari ambalo litatumika kusafirisha ama kutembeza watalii, linatakiwa libandikwe namba ya dharura ya 199.
Mbali na hayo Wizara pia imetoa mwongozo kwa wafanyakazi wa makampuni hayo, kuhakikisha wanapatiwa mafunzo maalum yanayohusiana na Corona, ikiwemo njia za kujizuia na kujikinga na maambukizi kama inavyoshauriwa na Wizara ya Afya.
Katika hatua nyingine Wizara pia imetoa mwongozo kwa viwanja vya ndege, kuhakikisha vinaweka mifumo ya kihabari viwanjani ili kuweza kutambua kama kuna mgonjwa yeyote ndani ya ndege na kutaka abiria wote wafanyiwe vipimo kabla ya kupanda ndege.
Post a Comment