Kutoka Daraja la Wami, zimetokea ajali mbili tofauti ambazo hazijapishana sana, moja ni ya Lori ambalo lilifeli breki na kutumbukia Mtoni na bado halijatolewa huku ikiaminika kuwa Dereva bado yupo ndani ya Lori hilo chini ya maji tangu Ijumaa June 05, 2020 ajali ilipotokea, wenzake wawili tayari wameokolewa .
Wakati Watu wakiwa wamejaa kushuhudia ajali hiyo ghafla Lori jingine pia likafeli breki na kuua Watu wawili (Mama na Mtoto) kisha kuyazoa magari zaidi ya sita ambayo yote yameharibika vibaya.
Post a Comment