Featured

    Featured Posts

KAMATI KUU YAMPONGEZA RAIS DK. MAGUFULI KWA UMAHIRI ALIOTUMIA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA CORONA, YARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2020

Dodoma, Tanzania
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imempongeza Rais Dk. John Magufuli kwa Uongozi imara, msimamo thabiti na usioyumba katika kipindi chote cha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid 19.

Pongezi hizo zimetolewa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, katika kikao chake kilichofanyika jana katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli.

Pamoja na pongezi hizo Kamati Kuu kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi, imeendelea kutoa rai kwa umma wa Watanzania kuendelea kuzingatia ushauri na maelekezo ya Serikali na wataalam wa Afya, kumtanguliza Mungu kwa maombi na shukrani katika kujikinga ya maabukizi ya virusi hivyo vya Corona huku wakiendelea kuchapa kazi kwa bidii.

"Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa  imepokea taarifa ya Serikali juu ya Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Korona na hatua ambazo zimechukuliwa kuukabili ugonjwa huo kwa mafanikio makubwa Nchini.

Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya Tafakuri ya kina juu ya Taarifa ya Serikali, kwa kauli moja kimempongeza Ndg. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Uongozi imara, msimamo thabiti na usioyumba katika kipindi chote cha mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Kamati Kuu na kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inaendelea kutoa rai kwa umma wa watanzania kuendelea kuzingatia ushauri na maelekezo ya Serikali na wataalam wa Afya, Kumtanguliza Mungu kwa maombi na shukrani na kuendelea kuchapa kazi kwa bidii", imesema sehemu ya Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole kuhusiana na yaliyojiri katika kikao hicho.

Katika taarifa hiyo, Polepole amesema pia kwamba Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa imepokea na kujadili Mpango wa Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na kwamba kwa kauli moja imeridhishwa na kiwango cha Maandalizi ya kuelekeza Uchaguzi huo na Kamati Kuu imeelekeza kutolewa maramoja kwa ratiba ya mchakato wa ndani wa uteuzi wa wana CCM wanaoomba kupewa dhamana ya uongozi katika vyombo vya Dola.

Kuhusu Maandalizi ya Mwelekeo wa Sera za CCM kwa Mwaka 2020 – 2030 na Ilani ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 Polepole amesema katika taarifa hiyo kwamba Kamati Kuu imepokea taarifa ya Maendeleo ya Uandishi wa Mwelekeo wa Sera za CCM kwa Mwaka 2020 – 2030 na kujiridhisha kuwa kazi nzuri imefanyika mpaka ngazi ya Rasimu ya Pili.

"Kamati Kuu pia imepitia kwa mara ya pili Taarifa ya Uandishi wa Ilani ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na imepongeza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa kujumuisha maoni ya wadau mbalimbali na kuelekeza maandalizi ya mwisho ili Ilani hiyo iwasilishwe katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kwa uamuzi wa mwisho", amesema Polepole katika taarifa hiyo. 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana