Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amevitaka vyuo vyote nchini kuhakikisha hadi kufikia ijumaa Juni 5, mwaka huu viwe vimeshawalipa wanafunzi wote fedha zao za kujikimu na ambao hawatafanya hivyo watachukuliwa hatua.
Waziri Ndalichako ameyasema hayo leo Juni 3, 2020 jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi magari manne kwa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambacho ni miongoni mwa vyuo vinne vitakavyonufaika na mkopo huo wa Benki ya Dunia kupitia mradi wao wa Kuleta Mapinduzi kwenye elimu ya ufundi Afrika Mashariki (EASTRIP).
Profesa Ndalichako amesema kuwa kuna baadhi ya vyuo mpaka leo bado havijawapatia wanafunzi fedha hizo za kujikimu licha ya kwamba Serikali imeshazitoa hivyo anatoa siku tatu kuanzia leo kuhakikisha wanazitoa ili wanafunzi waendelee na masomo bila kupata usumbufu wowote.
"Wanafunzi ikifika Ijumaa ya wiki hii mume mmeshalipwa fedha zenu na chuo ambacho hakitafanya hivyo hakuna msalia mtume, wizara yangu haitaweza kukivumilia kwa sababu hakuna sababu ya kuchelewesha kufanya malipo hayo kwa kuwa fedha tayari zilishapelekwa vyuoni," amesema Ndalichako.
Post a Comment