Hatimaye meli ya New Mv Victoria Hapa Kazi Tu iliyokuwa imesitisha huduma za usafiri katika ziwa victoria kati ya Mwanza na Kagera imetia nanga katika bandari ya Bukoba ikitumia muda wa takribani saa sita tofauti na saa 12 za awali..
Meli hiyo iliyokuwa ikijulikana kama MV Victoria imepokelewa jana katika bandari ya Bukoba majira ya saa 10 jioni june 28 mwaka huu na imeelezwa kuwa ilianza safari zake katika bandari ya Mwanza majira ya saa 3 asubuhi na kwamba ilisitisha huduma kati ya mwanza na Bukoba takribani miaka sita iliyopita.
Mgeni rasmi alikuwa ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole, ambaye alisafiri na meli hiyo kutoka Mwanza hadi Bukoba na emeeleza ujio wa meli hiyo ilivyo kielelezo tosha cha utekelezaji wa ahadi ya CCM na maono ya Rais John Pombe Magufuli kwa maendeleo ya watanzania,.
Pole pole amesema ameagizwa na Rais Magufuli kuwatangazia wakazi wa kanda ya ziwa kuwa gharama za kusafilisha mizigo zitakuwa ndogo kulinganisha na hapo awali ambapo tani moja itasafirishwa kwa sh elfu 27 tofauti na ilivyokuwa awali ya sh 120,000 kwa mzigo wa tani moja
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kagera Bregidia General Marco Gaguti amesema kuwa ujio wa meli hiyo utafunguia fursa za kibiashara baina ya Kagera na mikoa jirani pamoja na nchi zinazozunguka mkoa wa kagera
Post a Comment