Mwili wa aliyekuwa rais wa Burundi hayati Pierre Nkurunziza unazikwa leo kwenye makaburi ya mji wa Gitega ,mji mkuu wa kisiasa ulioko katikati mwa Burundi
Hafla ya mazishi zinatarajiwa kuongozwa na rais mpya jenerali Evariste Ndayishimiye na wakuu wengine wa serikali.
Hayati Nkurunziza alifariki dunia tarehe 8 mwezi huu ,miezi miwili kabla ya kukabidhi madaraka kwa mrithi wake kufwatia uchaguzi uliofanyika mwezi wa tano.
Kwa mjibu wa tangazo lililotolewa na serikali ya Burundi, hafla itaanzia kwenye 'hospital du Cenquantenaire Twese Turashoboye' iliyoko kwenye mkoa wa Karusi ambako maiti yake imehifadhiwa.
Mlolongo wa magari yatakayosindikiza maiti yake utatoka kwenye hospitali hiyo utatoka Karusi na kuelekea katika mji wa Gitega ambao ni mji mkuu wa kisiasa katikati mwa Burundi.
Wananchi wameomba kusimama kwenye barabara kumuaga marehemu.
Kunatarajiwa hafla fupi ya jeshi kumtolea heshma za mwisho kwenye uwanja wa mpira wa Ingoma mjini Gitega,kabla ya mwili wake kupitishwa mbele ya wananchi watakaokuwa uwanjani humo kumwaga na baadae kufanyika maziko rasmi.
Tangazo la serikali ya Burundi linasema kwamba shughuli nyingine kama kuweka mashada ya maua kwenye kaburi lake au hotuba zitakazotolewa zitafahamishwa leo.
Rais Pierre Nkurunziza alifariki dunia tarehe 8 mwezi huu kutokana na mshtuko wa moyo kama ilivyotangazwa na serikali ya nchi hiyo.
Nkurunziza ni nani?
Pierre Nkurunziza amekuwa mwanasiasa wa Burundi na kuwa madarakani tangu mwaka 2005.
Bwana Nkurunziza, kijana wa aliyekuwa mbunge, alinusurika mauaji 1993 ya wanafunzi wa Kihutu katika chuo kiuu cha Burundi ambapo alikuwa mhadhiri na kujiunga na waasi wa FDD kundi ambalo baadae lilibadilika na kuwa chama tawala cha CNDD-FDD ambacho alikuja akawa kiongozi.
Alikuwa mwenyekiti wa chama tawala cha CNDD-FDD, hadi alipochaguliwa kama rais wa Burundi.
Baada ya makubaliano ya Amani ya Arusha kati ya serikali na waasi, Nkurunziza alitajwa kuwa waziri wa mambo ya ndani kabla ya bunge kumchagua kama rais Agosti 2005.
2015, Nkurunziza alichaguliwa katika uchaguzi uliokuwa na utata na chama chake kwa muhula wa tatu madarakani.
Wafuasi wake na wanaompinga Nkurunziza walikosa kukubaliana katika suala la ikiwa ilikuwa halali kwake kugombea tena na maandamano yakafuata.
Post a Comment