Rais Magufuli amempongeza Evariste Ndayishimiye kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Burundi katika uchaguzi uliofanyika Mei 20. 2020.
Rais Magufuli ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter, na kuongeza kuwa wananchi wa Burundi wameonesha imani kubwa kwa kumchagua kiongozi hiyo.
“Nakupongeza Ndg. Evariste Ndayishimiye kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Burundi. Wananchi wa Burundi wameonesha imani kubwa kwako,” ameandika Rais Magufuli.
Post a Comment