Featured

    Featured Posts

TRUMP AFICHWA KATIKA HANDAKI KUHOFIA MAANDAMANO YA KIFO CHA MMAREKANI MWEUSI GEORGE FLOYD.

Usalama umeimarishwa katika Ikulu ya Whitehouse katika siku za hivi karibuni

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionUsalama umeimarishwa katika Ikulu ya Whitehouse katika siku za hivi karibuni
Maandamano na ghasia kufuatia kifo cha George Floyd yaliikaribia Ikulu ya Whitehouse.
Tangu wiki iliopita, makao makuu ya ofisi hiyo na makaazi ya rais wa Marekani yalikuwa kitovu cha maandamano makubwa zaidi kufanyika nchini humo tangu yale yaliofanyika baada ya mauaji ya Martin Luther King 1968.
Kifo cha Floyd baada ya afisa wa polisi kumwekea goti katika shingo yake kwa zaidi ya dakika nane kimezua wimbi la ghasia ambazo zimeenea hadi katika miji 75 , ikiwemo mji mkuu na maeneo yalio karibu na makaazi ya rais.
Siku ya Jumatatu , huku rais Trump akitangaza kwamba atapeleka jeshi iwapo ghasia zitazidi, kulikua na sauti za kelele wakati alipokuwa akitoa hotuba yake kwa taifa.
Muda mfupi baadaye makumi ya waandamanaji walipigwa na kunyunyiziwa vitoa machozi ili kuwaondoa katika eneo hilo ambapo baadaye rais huyo alijitokeza na kupiga picha akiwa ameshikilia biblia katika kanisa ambalo lilikuwa limeharibiwa mkesha wa siku hiyo.
Karibu na ikulu ya whitehouse kulikuwa na maandamano ya ghasiaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKaribu na ikulu ya whitehouse kulikuwa na maandamano ya ghasia
Na sasa imebainika kwamba wikendi iliopita , wakati Ikulu ya Whitehouse ilipofungwa kwa dharura kutokana na maandamano hayo , inadaiwa kwamba rais huyo alichukuliwa na kufichwa chini ya handaki lililojengwa zaidi ya nusu karne iliopita chini ya eneo moja la Ikulu hiyo.
Siku ya Ijumaa , hatahivyo, Trump alikataa kwamba alikuwa amefichwa katika handaki hilo kutokana na maandamano na kwamba alikuwa amepelekwa katika eneo hilo ili kulikagua .
Hatahivyo alama ya reli iliokuwa ikisambaa ya #bunkerboy ilisambazwa kwa siku kadhaa na vyombo vya habari nchini humo vilizungumzia ratiba ambayo haikuwahi kusikika tangu shambulio la 11, 2001.
Je nini kinachojulikana kuhusu handaki hilo?
Kulingana na data na picha zilizofichuliwa, ni eneo lililo chini ya ardhi magharibi mwa wingi ya Ikulu ya Whitehouse , Ujenzi wake ulifanyika 1942 , muda mfupi bada ya vita vya pili vya dunia na lililenga kutoa ulinzi kwa rais aliyekuwepo Franklin D Roosevelt dhidi ya shambulio la adui kutoka angani mjini Washington
Trump akiwa katika chumba cha mikutano kinachotumika na rais kutoa maagizo chini ya ikulu ya WhitehouseHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTrump akiwa katika chumba cha mikutano kinachotumika na rais kutoa maagizo chini ya ikulu ya Whitehouse
Kulingana na vyombo vya habari , limetenegenezwa kutokana na nyuta zilizo na saruji nzito zinazoweza kuhimili shambulio la kinyuklia ama hata athari za moja kwa moja za ndege na lina mfumo wa hewa na hifadhi ya chakula ambacho kinaweza kutumika kwa miezi kadhaa.
Katika kitabu chake cha 'Spoken from the heart', Laura Bush , mkewe aliyekuwa rais wa Marekani George W Bush anasema kwamba handaki hilo limejengwa hali ya kwamba ni kama kituo cha kutoa maagizo na kwamba kina runinga, simu ,na vifaa vya mawasiliano.
Picha zilizotolewa na serikali zinaonyesha kwamba handaki hilo lina chumba cha mikutano , kituo cha kutoa maagizo ambacho rais na kundi lake atafanya kazi wakati wa hali ya dharura.
Laura Bush anasema kwamba alipelekwa katika jumba hilo la ardhini wakati wa shambulio la Septemba 11 2001.
Je handaki hilo limetumika mara ngapi?
Mara ya kwanza handaki hilo lilipotumika ni wakati wa shambulio la Septemba 11 2011 , wakati ndege zilizotekwa na kundi la wapiganaji wa al-Qaeda ziligonga majumba mawili marefu mjini New York na jengo la Pentagon , kilomita chache kutoka ikulu ya Whitehouse.
MojawapoHaki miliki ya pichaNATIONAL ARCHIVE
Siku hiyo makamu wa rais Richard Cheney waziri wa maswala ya kigeni Condoleeza Rice, na washauri kadhaa walikimbizwa katika handaki hilo.
Kulingana na ripoti ya Septemba 11 kutoka kwa tume , iliochapishwa tarehe 22 Julai 2004, uamuzi wa kuwapeleka maafisa wakuu wa serikali , katika handaki hilo ulifanyika baada ya ndege moja iliokuwa imetekwa kubadilisha njia na kuelekea katika Ikulu ya whithouse.
Habari hiyo ilishinikiza kikosi cha secret Service kumuagiza makamu wa rais kuondolewa haraka kabla ya mwendo wa saa 9.36 asubuhi.
Kulingana na ripoti rasmi , Cheney alisimama katika eneo moja la handaki hilo ambalo lilikua na simu , benki na runinga na kuomba kuzungumza na rais , lakini ilichukua muda mwingi kuunganisha simu hiyo.
Vyombo vya habari Marekani vinasema kwamba shambulio hilo lilifichua kwamba vifaa vya mawasiliano katika mahandaki mengi havifanyi kazi vizuri, hivyobasi vilihitaji kufanyiwa mabadiliko miaka kdhaa baadaye.
Cheney alikimbizwa katika handaki hiloHaki miliki ya pichaNATIONAL ARCHIVE
Image captionCheney alikimbizwa katika handaki hilo
Hatahivyo hakuna rekodi nyengine kwamba handaki hil lilitumika tena katika tukio la dharura tangu miaka ya mapema ya vita dhidi ya ugaidi.
Gazeti la The Washington post linahakikisha kwamba muda mfupi baada ya kuteuliwa Januari 2017, Trump alipelekwa katika handaki hilo ili kujifunza kuhusu lilivyojengwa na operesheni yake kama mafunzo ambayo rais mpya anapata kutoka katika Ikulu ya whitehouse.
Miaka mitatu baadaye , kulingana na vyombo vya habari alihamishwa katika eneo hilo kwa dharura, lakini sio kwa shambulio la adui ama ugaidi bali kutokana na maandamano ya raia waliomchagua.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana