George Floyd, raia mweusi wa Marekani ambaye kifo chake kimesababisha maandamano makubwa Marekani, alikufa kutokana na ukosefu wa hewa safi ya (oksijeni), kwa mujibu wa uchunguzi binafsi wa maiti yake.
Alifariki kwa kukandamizwa kwa goti shingoni na mgongoni na maafisa wa polisi wa Minneapolis, uchunguzi wa kimatibabu uliosimamiwa na familia ya Floyd umebaini hilo.
Matokeo hayo yanatofautiana na matokeo ya uchunguzi wa mwili wake uliofanywa na madktari wa kaunti.
Kulingana na matokeo hayo, hakukupatikana ushahidi wowote unaohusisha ukosefu wa hewa wala kunyongwa.
Matokeo ya uchunguzi huo wa kimatibabu pia yalibaini kwamba matatizo ya afya yalichangia pakubwa kifo cha Bwana Floyd.
Lakini madaktari waliosimamiwa na familia ya Floyd walibaini kwamba kifo chake kilikuwa ni mauaji, taarifa kutoka kwa timu yake ya sheria inasema.
"Sababu ya kifo kwa maoni yangu kimesababishwa na ukosefu wa hewa, kutokana na kukandamizwa shingoni ambako kunaweza kutatiza oksijeni inayokwenda kwenye ubongo - na kupelekea mkandamizo mgongoni, ambako kuna tatiza upumuaji," Dkt. Michael Baden, aliyekuwa daktari wa mji wa New York pamoja na mwengine wamesema katika mkutano na wanahabari.
Video inayoonesha afisa wa polisi mzungu akiendelea kupiga goti juu ya shingo ya George Floyd hata baada ya kusema kwamba anashindwa kupumua imesababisha hasira na ghadhabu miongoni mwa raia tangu ilipoonekana wiki moja iliyopita.
Tukio hilo limesababisha maandamano ya siku sita mfululizo kote Marekani na machafuko ambayo hayajawahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa katika maeneo mbalimbali nchini humo.
Benjamin Crump, wakili wa familia Floyd, Jumatatu amesema katika mkutano na wanahabari:
''Bila shaka leo hii leo angekuwa hai ikiwa hangekumbana na shinikizo ya namna ile kwenye shingo yake kuliko sababishwa na Derek Chauvin aliyekuwa afisa wa polisi pamoja na mvutano uliotokea kutoka kwa maafisa wengine wawili."
Aliongeza kwamba: " Ambulansi ilikuwa gari ya kubeba maiti yake."
Dkt. Baden anasema hakuwa na tatizo jingine lolote la afya ambalo huenda lingesababisha au kuchangia kutokea kwa kifo chake".
Matokeo ya uchunguzi huo yana hitilafiana na yale ya uchunguzi wa awali yaliyojumuishwa kwenye malalamishi ya uhalifu dhidi ya Bwana Chauvin, ambaye ameshtakiwa kwa mauaji ya kiwango cha tatu na kuua bila kukusudia.
Utafiti wa matibabu ulisema katika ripoti hiyo kwamba Bwana Floyd alikuwa na matatizo ya moyo na kusema kuwa yote hayo yakijumuishwa pamoja, yalikuwa na uwezo wa kutatiza mfumo wake na shinikizo kutoka kwa maafisa huenda kulisababisha kifo chake."
Matokeo kamili ya uchunguzi wa kifo chake bado hayajatolewa na ofisi ya matibabu ya kaunti ya Hennepin. Inasema kuwa inasubiri matokeo zaidi kutoka katika maabara.
Falimia ya Floyd na wawili wao inasema mashtaka dhida ya Bwana Chauvin yanastahili kuongezwa hadi kiwango cha kwanza cha mauaji.
Wanasema uchunguzi binafsi wa maiti yake unathibitisha kwamba maafisa wengine wawili waliochukua video wakati raia huyo mweusi anakandamizwa shingoni kwa goti pia nao walichangia kifo chake.
Yapi mapya katika maandamano hadi kufikia sasa?
Zaidi ya miji 75 imekumbwa na maandamano kwasababu ya kifo cha George Floyd, mitaa ikiwa imefurika watu wanaoandamana bega kwa bega siku chache tu baada ya mitaa hiyo kuwa bila hata mmoja kwasababu ya ni virusi vya corona.
Tukio la kuuawa kwa Floyd limesababisha hasira kwa jinsi maafisa wa polisi wanavyotekeza mauaji dhidi ya raia weusi ni na vitendo vya ubaguzi wa rangi.
Mauaji hayo yanafuatia yale ya Michael Brown huko Ferguson, Eric Garner, New York na wengine ambako kumepelekea kuanzishwa kwa vuguvugu la 'Maisha ya mtu mweusi pia ni muhimu'
Jumapili, yale ambayo yalikuwa ni maandamano ya amani yaligeuka na kuwa ghasia katika miji mingi, huku vurugu zikizuka kati ya maafisa wa polisi na waandamanaji.
Magari ya maafisa wa polisi na majengo yalichomwa moto na maduka kuporwa kwenye maeneo kadhaa. Miji mingi imeweka hatua ya kutoka nje lakini agizo hilo linakiukwa.
Jumatatu, rais Trump aliwaambia magavana wa majimbo kwamba wamelegeza kamba mno na wakati unawadia wa kuchukua hatua stahiki na kutumia vizuri vikosi kutoka Jeshi la Taifa, ambapo maelfu yao tayari wamepelekwa katika majimbo mawili.
"Munatakiwa kukamata watu, munatakiwa kutafuta watu na kuwafunga gerezani kwa miaka 10 na hamutawahi kushuhudia tena kitu kama hiki," Bwana Trump alisema katika mkutano wa njia ya video, kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.
Kumekuwa na matukio ya ghasia katika mji wa Washington DC nyakati za usiku hivi karibuni, pamoja na eneo karibu na Ikulu ya Marekani.
Lakini raia weusi wa Marekani wanachukuliwa vipi?
Waandamanaji wanawasha moto majengo ikiwemo kanisa la kihistoria linalofahamika kama kanisa la rais usiku wa Jumapili.
Video nyingi zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii kote Marekani zinaonekana kuonesha polisi wa kukabiliana na ghasia wakitumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji. Mashumbulizi kadhaa yanayolenga wanahabari pia yameripotiwa.
Hatua ya kutotoka nje katika mji wa Washington DC imeongezwa kwa siku mbili usiku na itaanza kuanzia saa moja usiku Jumatatu. Hatua hiyo pia ilitekelezwa Jumapili kuanzia taa tano usiku.
Mji wa New York pia nao unaweka hatua ya kutotoka nje kuanzia Jumatatu kuanzia saa tano usiku hadi kumi na moja asubuhi Jumanne.
George Floyd, raia mweusi wa Marekani ambaye kifo chake kimesababisha maandamano makubwa Marekani, aliaga dunia kwasababu ya ukosefu wa hewa safi ya (oksijeni), kwa mujibu wa uchunguzi binafsi wa maiti yake.
Aliaga dunia kwa kukandamizwa shingoni na mgongoni na maafisa wa polisi wa Minneapolis, uchunguzi wa kimatibabu uliosimamiwa na familia ya Floyd umebaini hilo.
Matokeo hayo yanatofautiana na matokeo ya uchunguzi wa maiti yake uliofanywa na madktari wa kaunti.
Kulingana na matokeo hayo, hakukupatikana ushahidi wowote unaohusisha ukosefu wa hewa wala kunyongwa.
Unaweza pia kutazama:
Matokeo ya uchunguzi huo wa kimatibabu pia yalibaini kwamba matatizo ya afya yalichangia pakubwa kifo cha Bwana Floyd.
Lakini madaktari waliosimamiwa na familia ya Floyd walibaini kwamba kifo chake kilikuwa ni mauaji, taarifa kutoka kwa timu yake ya sheria inasema.
"Sababu ya kifo kwa maoni yangu kimesababishwa na ukosefu wa hewa, kutokana na kukandamizwa shingoni ambako kunaweza kutatiza oksijeni inayokwenda kwenye ubongo - na kupelekea mkandamizo mgongoni, ambako kuna tatiza upumuaji," Dkt. Michael Baden, aliyekuwa daktari wa mji wa New York pamoja na mwengine wamesema katika mkutano na wanahabari.
Video inayoonesha afisa wa polisi mzungu akiendelea kupiga goti juu ya shingo ya George Floyd hata baada ya kusema kwamba anashindwa kupumua imesababisha hasira na ghadhabu miongoni mwa raia tangu ilipoonekana wiki moja iliyopita.
Tukio hilo limesababisha maandamano ya siku sita mfululizo kote Marekani na machafuko ambayo hayajawahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa katika maeneo mbalimbali nchini humo.
Benjamin Crump, Wakili wa familia Floyd, Jumatatu amesema katika mkutano na wanahabari:
''Bila shaka leo hii leo angekuwa hai ikiwa hangekumbana na shinikizo ya namna ile kwenye shingo yake kuliko sababishwa na Derek Chauvin aliyekuwa afisa wa polisi pamoja na mvutano uliotokea kutoka kwa maafisa wengine wawili."
Aliongeza kwamba: " Ambulansi ilikuwa gari ya kubeba maiti yake."
Dkt. Baden anasema hakuwa na tatizo jingine lolote la afya ambalo huenda lingesababisha au kuchangia kutokea kwa kifo chake".
Matokeo ya uchunguzi huo yana hitilafiana na yale ya uchunguzi wa awali yaliyojumuishwa kwenye malalamishi ya uhalifu dhidi ya Bwana Chauvin, ambaye ameshtakiwa kwa mauaji ya kiwango cha tatu na kuua bila kukusudia.
Utafiti wa matibabu ulisema katika ripoti hiyo kwamba Bwana Floyd alikuwa na matatizo ya moyo na kusema kuwa yote hayo yakijumuishwa pamoja, yalikuwa na uwezo wa kutatiza mfumo wake na shinikizo kutoka kwa maafisa huenda kulisababisha kifo chake."
Matokeo kamili ya uchunguzi wa kifo chake bado hayajatolewa na ofisi ya matibabu ya kaunti ya Hennepin. Inasema kuwa inasubiri matokeo zaidi kutoka katika maabara.
Falimia ya Floyd na wawili wao inasema mashtaka dhida ya Bwana Chauvin yanastahili kuongezwa hadi kiwango cha kwanza cha mauaji.
Wanasema uchunguzi binafsi wa maiti yake unathibitisha kwamba maafisa wengine wawili waliochukua video wakati raia huyo mweusi anakandamizwa shingoni kwa goti pia nao walichangia kifo chake.
Yapi mapya katika maandamano hadi kufikia sasa?
Zaidi ya miji 75 imekumbwa na maandamano kwasababu ya kifo cha George Floyd, mitaa ikiwa imefurika watu wanaoandamana bega kwa bega siku chache tu baada ya mitaa hiyo kuwa bila hata mmoja kwasababu ya ni virusi vya corona.
Tukio la kuuawa kwa Floyd limesababisha hasira kwa jinsi maafisa wa polisi wanavyotekeza mauaji dhidi ya raia weusi ni na vitendo vya ubaguzi wa rangi.
Mauaji hayo yanafuatia yale ya Michael Brown huko Ferguson, Eric Garner, New York na wengine ambako kumepelekea kuanzishwa kwa vuguvugu la 'Maisha ya mtu mweusi pia ni muhimu'
Jumapili, yale ambayo yalikuwa ni maandamano ya amani yaligeuka na kuwa ghasia katika miji mingi, huku vurugu zikizuka kati ya maafisa wa polisi na waandamanaji.
Magari ya maafisa wa polisi na majengo yalichomwa moto na maduka kuporwa kwenye maeneo kadhaa. Miji mingi imeweka hatua ya kutoka nje lakini agizo hilo linakiukwa.
Jumatatu, rais Trump aliwaambia magavana wa majimbo kwamba wamelegeza kamba mno na wakati unawadia wa kuchukua hatua stahiki na kutumia vizuri vikosi kutoka Jeshi la Taifa, ambapo maelfu yao tayari wamepelekwa katika majimbo mawili.
"Munatakiwa kukamata watu, munatakiwa kutafuta watu na kuwafunga gerezani kwa miaka 10 na hamutawahi kushuhudia tena kitu kama hiki," Bwana Trump alisema katika mkutano wa njia ya video, kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.
Kumekuwa na matukio ya ghasia katika mji wa Washington DC nyakati za usiku hivi karibuni, pamoja na eneo karibu na Ikulu ya Marekani.
Lakini raia weusi wa Marekani wanachukuliwa vipi?
Waandamanaji wanawasha moto majengo ikiwemo kanisa la kihistoria linalofahamika kama kanisa la rais usiku wa Jumapili.
Video nyingi zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii kote Marekani zinaonekana kuonesha polisi wa kukabiliana na ghasia wakitumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji. Mashumbulizi kadhaa yanayolenga wanahabari pia yameripotiwa.
Hatua ya kutotoka nje katika mji wa Washington DC imeongezwa kwa siku mbili usiku na itaanza kuanzia saa moja usiku Jumatatu. Hatua hiyo pia ilitekelezwa Jumapili kuanzia taa tano usiku.
Mji wa New York pia nao unaweka hatua ya kutotoka nje kuanzia Jumatatu kuanzia saa tano usiku hadi kumi na moja asubuhi Jumanne.
Trump aahidi kutuma vikosi
Wakati huohuo, rais wa Marekani Donald Trump ameahidi kutuma vikosi kumaliza maandamano.
Tishio hilo linawadia wakati maandamano yanazidi kuongezeka kote nchini humo, kufuatia kifo cha George Floyd, Mmarekani mweusi aliyekufa mikononi mwa polisi.
Bwana Trump amesema kuwa ikiwa miji na majimbo yatashindwa kutuliza hali na kudhibiti waandamanaji kwa kutetea wakaazi wake, atapeleka jeshi na kuwatatulia tatizo hilo kwa haraka.
Kifo cha George Floyd, 46, huko Minneapolis kilichotokea Mei 25 kimesababisha ghadhabu kote nchini humo hii leo ikiwa maandamano hayo yanaingia siku ya saba na kuonesha uwezekano mkubwa wa kuendelea.
Trump alisema nini?
Katika Ikulu ya Marekani kwenye Bustani ya Rose Jumatatu jioni, Trump alisema
" Raia wote wa Marekani wameshtushwa na kifo cha George Floyd, lakini kumbukumbu hiyo haistahili kuondolewa na raia wenye ghadhabu".
Bwana Trump alielezea matukio ya uporaji na ghasia katika mji mkuu Jumapili kama aibu na kutaka usalama kuimarishwa.
"Napeleka maelfu na maelfu ya wanajeshi wenye silaha, maafisa wa jeshi na maafisa wa utekelezaji sheria kusitisha uporaji, ghasia, mashambulizi na uharibifu wa mali unaoendelea," alisema.
Bwana Trump kisha akarejesha angalizo kwa maandamano yanayoendelea nchini humo, na kutupia kidole cha lawama wanaotaka kuangusha serikali.
Bwana Trump aliongeza kwamba: ''Ikiwa mji au jimbo litakataa kuchukua hatua stahiki… nitapeleka jeshi na kutatua tatizo hilo tena kwa haraka.''
"Nataka wanaopanga ugaidi huu watambue kwamba mutakabiliana na makosa kadhaa ya uhalifu," aliongeza.
Matamshi yake yalikosolewa na mwanachama mwandamizi wa Democrats, Joe Biden, ambaye huenda akapeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang'anyiro cha urais, na kusema Bwana Trump anatumia jeshi la Marekani dhidi ya raia wa Marekani.
Kiongozi wa walio wachache katika bunge la Seneti Chuck Schumer alisema: "rais huyu anaweza kujidunisha kiasi gani?... Matendo yake yanaonesha uhalisia wake."
Post a Comment