CCM Blog, Kigoma
SHIRIKA la Umeme Tanesco kupitia idara yake ya masoko imeendesha kampeni ya kuhamasisha wananchi wa mkoa wa Kigoma kuchangamkia fursa ya kuwekewa umeme wa REA ambao mkandarasi bado anaendelea na kazi kwenye vijiji mbalimbali mkoani hapa.
Elimu hiyo iliyoanza kutolewa kwenye mkoa huo wili hii imewafikia wanakijiji wa vijiji vya Kigoma ambapo baadhi ya wananchi wameishukuru serikali kwa miradi hii ya kuunganishiwa umeme wa bei nafuu kwani inachangia maendeleo ya kiuchumi.
Vijiji ambavyo tayari vimeshapatiwa Elimu ni Buhigwe Katundu, Kajana, Kinazi, Chankere, Bubango, Kizega, Kishanga, Munze na Mnanila. Kuunganisha umeme ni shilingi elfu 27,000 tu. KUONA MATUKIO KATIKA PICHA>>BOFYA HAPA
Post a Comment