Featured

    Featured Posts

WAZIRI MHAGAMA AMEKUTANA NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI MKOANI MANYARA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi kuhusu masuala mbalimbali ya wafanyakazi walipokutana katika ukumbi wa Hazina ndogo, Mkoani Manyara.
Sehemu ya Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wa Mkoa wa Manyara wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipokutana nao na jadiliana masuala mbalimbali kuhusu wafanyakazi.
Mratibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Mkoa wa Manyara Bw. Kombo Kombo (kushoto) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo walipokutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati). Wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Manyara Mhe. Elizabeth Kitundu (kulia) Kaimu Katibu Tawala Bw. Said Mabie. Wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Manyara, Bw. Wenseslaus Musenya.
 Mkuu wa Wilaya ya Manyara Mhe. Elizabeth Kitundu akieleza jambo wakati wa Mkutano huo.
Mwakilishi wa Kamati ya Utendaji kutoka Chama Cha Walimu (CWT) Mkoa wa Manyara Bw. Elias Iyo akieleza jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Hazina ndogo, Mkoani Manyara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wa Mkoa Manyara alipokutana nao na kuzungumza masuala mbalimbali ya wafanyakazi. Kulia ni aliyekuwa Mbunge wa Babati Vijijini Mhe. Vrajilal Jituson.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
OWM – KVAU
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana