Featured

    Featured Posts

BENKI YA NMB YATOA MILIONI 42.5 MAONYESHO YA NANENANE SIMIYU



Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi – Sospeter Magesse akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. Milioni 42.5 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu- Festo Kiswaga (kulia), ikiwa ni mchango wa benki hiyo kwa ajili ya  Maonyesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika viwanja vya Nyakabindi Mkoani humo. (Katikati) ni Katibu Tawala wa Mkoa – Mariam Mmbaga na Meneja wa NMB Tawi la NMB Bariadi – Gabriel Paul.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi – Sospeter Magesse (kushoto) akimkabidhi Tisheti Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu – Festo Kiswaga (kulia), kama udhamini wa Benki hiyo katika Maonyesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika viwanja vya Nyakabindi Mkoani humo.
………………………………………………………………………………………….
Benki ya NMB imetoa Shilingi Milioni 42,500,000 kwa ajili ya kudhamini maonyesho ya Nanenane ya yatakayofanyika kitaifa Kanda ya Magharibi  katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu kuanzia tarehe 01 hadi 08 Agosti, 2020 kwa  kauli mbiu isemayo “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020“.
Pamoja na kiasi hicho cha pesa, Benki hiyo imekabidhi T-shirt 300 zitakazotumika kwenye maonyesho hayo, ikiwa ni moja ya udhamini wake. Huu ni mwaka wa tatu mfululizo Benki ya NMB inadhamini Maonyesho hayo.

Akikabidhi mfano wa hundi ya Sh. Mil 42.5 kwa uongozi wa Mkoa wa Simiyu Meneja wa benki hiyo Kanda ya Magharibi- Sospeter Magesse alisema, Benki ya NMB kusaidia sekta ya kilimo ni fahari kwao kwani kupitia kilimo benki imekuwa ikifanya biashara kubwa ambayo imechangia kukua kwa sekta hiyo.

“Kwa miaka mitatu ambayo maonesho hayo yamefanyika Mkoani Simiyu,tayari NMB tumetoa udhamini wa zaidi ya Mil 100, hii ni katika kuhakiksha sekta hii inakuwa imara na kuongeza pato la taifa,” alisema Magesse

“Katika kuunga mkono juhudi za Rais wetu wa awamu ya tano,Dkt John Magufuli kwa miaka mitano ya awamu ya tano ya serikali yake,mchango wetu kama benki tumeweza kujenga uchumi imara kupitia kilimo na ufugaji” Magesse.

Aliongeza kuwa ndani ya miaka miwili Benki hiyo imefanikiwa kufungua akaunti 500,000 za wakulima ambapo kwa Mkoa wa Simiyu jumla za akaunti 86,000 za wakulima wa pamba zimefunguliwa.

Meneja huyo alisema kuwa kama Benki kinara nchini itaendelea na iko tayari  kuendeleza uhusiano wenye manufaa kati yao ,wakulima, wafugaji na wadau wengine wa kilimo ili watumie fursa vizuri zilizopo kwenye soko na kukuza mitaji ya biashara zao.

Akipokea mchango huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo – Antony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi- Festo Kiswaga  ameishukuru Benki hiyo kwa namna ambavyo wanajitoa kusaidia maendeleo ya wananchi hususani wakulima ambao ndio chanzo kikuu cha ukuwaji wa uchumi wa nchi, ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa elimu ya kilimo bora kwa wakulima, kuwapatia mikopo  na kuwafungulia akaunti wakulima.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana