Unapotaja Wanawake wachapakazi, jasiri na walio imara katika maamuzi muhimu ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi, bila shaka huwezi kuacha kumtaja Mheshimiwa Hawa Mchafu Chakoma kwa kuwa ni miongozi mwa wanawake wa aina hiyo.
Bila shaka sifa hizo na ile ya kuwa kada mahiri katika CCM na Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) ni miongoni mwa sifa zilizomuwezesha kuwa Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Pwani kupitia Wafanyakazi.
Miongoni kwa sifa zinazoweza kudhihirisha uchapakazi, ujasiri katika maamuzi na kutekeleza majukumu ya ujenzi wa Taifa kwa upande wa Mbunge, nikueleza au kutoa taarifa ya ushiriki wake katika utekelezaji wa wa Ilani ya CCM katika kipindi ambacho amepewa dhamana ya nafasi hiyo kupitia viti maalum au kuchaguliwa katika jimbo.
Naye Mheshimiwa Hawa Mchafu Chakoma ametayarisha Taarifa hiyo kulingana na maelekezo ya Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ambalo ndio chombo kikuu cha maamuzi ya Umoja wa wanawake wakiwemo Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Hivyo basi kutokana na utaratibu uliotolewa na Baraza hilo kwa kila Mbunge ambaye ni mwanachama wa UWT kuandaa na kuwasilisha ripoti ya kazi ya utekelezaji wa ilani ya CCM. Taarifa ya Mheshimiwa Hawa Mchafu Chakoma imeainisha mambo mbalimbali ikiwemo yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli. Tafadhali isome taarifa hiyo hatua kwa hatua... BOFYA HAPA
Post a Comment