MWENYEKITI wa CCM Taifa Dkt. John Pombe Magufuli amepigiwa kura za ndiyo kwa asilimia 100 na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho kupeperisha bendera ya kuwania nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku Dkt Hussein Mwingi akiwa mgombea wa Zanzibar
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kura zilizopigwa ni 1,822 kati ya Wajumbe 1,822 za wajumbe wote waliohudhuria huku kukiwa hakuna kura iliyoharibika.
Akizungumza mara baada ya matokeo kutangazwa ndiye mpeperusha bendera wa Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu ujao, Magufuli amesema kura alizopata zinampa ari ya kuwatumikia zaidi Watanzania.
“Kura nilizopata leo zisinipe kiburi, zikanifanya nijione naweza sana kuliko wengine bali zinifanye niheshimu watu, niwatumikie wanyonge na Watanzania wote bila kubagua dini kabila wala rangi zao,
“nimefurahi sana na ndo maana ninasema nimebaki na deni kubwa sana na sitawaangusha kwa sababu ya imani mliyonipa.” Amesema Dkt.Magufuli
Magufuli pia mewashukuru wanachama wa CCM waliomdhamini na ambao hawakumdhamini kwa sababu ya kukosa fomu kwa wingi wao waliojitokeza kumdhamini.
“Nimedhaminiwa na wanachama zaidi ya milioni moja, lakini pia wengi walikosa fomu, napenda niwahakikishie ndugu zangu siku zote nitabaki kuwa mtumishi wenu.” Amesisitiza
Pia amesema kura hizo ziwe chachu hata kwa wasaidizi wake kuona kwamba wana wajibu wa kutenda matamanio ya watu. Amewakumbusha na watakaochaguliwa kuwa wana wajibu mkubwa wa kuwatumikia Watanzania.
“Ndugu zangu mmenipa kura kwa asilimia 100 lakini tusijiamini kwamba tunakwenda kushinda kwa asilimia 100, tukafanye kampeni kwa nguvu zote wakati ukifika kwa ajili ya Rais, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani, sasa ndio kumekucha kuhakikisha chama chetu kinaendelea kushika dola kwa nguvu zote na Wajumbe wa mkutano Mkuu tuna wajibu kukisaidia chama chetu kushinda, walioonyesha nia, uteuzi ndani ya chama ukikamilika tukaonyeshe umoja, Pia ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wanachama wa chama hicho kuhakikisha wanamchagua Dkt.Mwinyi katika Uchaguzi Mkuu ili aendelee kuijenga Zanzibar.
” Nawahakikishia mkiamchagua Mwinyi Zanzibar itapaa zaidi na mimi nitamsaidia kwa nguvu zangu zote kwa sababu najua ni mdogo wangu,
“kanichagulieni mtu ambaye nitajisikia raha, msinichagulie shikamoo, mtanipa shida na mimi nataka nije Zanzibara kwa raha zote.” Amesema
Aidha amewathibitishia viongozi wa upinzani kuwapa ushirikiano katika kampeni za uchaguzi.
“Sisi sote tunajenga nyunba moja, tuendelee kushikamana, tusitukanane majukwani, tufanye kampeni za kistaarabu na wapiga kura wetu wataamua.” Alimaliza Mgombea mteule wa Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa kupitia CCM, Dkt Magufuli.
Post a Comment