Featured

    Featured Posts

RAIS DK. MAGUFULI ATEUA RC, KATIBU MKUU, NAIBU KATIBU MKUU NA DC, LEO ASUBUHI

IKULU, Chamwino.
Rais Dk. John Magufuli leo tarehe 17 Julai, 2020 amefanya uteuzi wa viongozi wapya ambao ni  Dkt. Jumanne Fhika kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, ambaye kabla ya uteuzi huo, alikuwa Ofisi ya Rais na anachukua nafasi ya Bw. Christopher Ole Sendeka.

Dk. Aloyce Nzuki kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na kabla ya uteuzi huo, alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, anachukua nafasi ya Prof. Adolf Mkenda, Mhandisi Anthony Sanga kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji ambapo kabla ya uteuzi huo, alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji hiyo anachukua nafasi ya Prof. Kitila Alexander Mkumbo.

Taarifa ya Ikulu imewataja wateule wengine kuwa ni Dk. Allan Kijazi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuchukua nafasi ya Dk. Aloyce Nzuki aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, na kwamba Dk. Allan Kijazi ataendelea kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Pia Mhandisi Nadhifa Kemikimba ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji ambapo kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Kemikimba alikuwa Mkurugenzi katika Wizara ya Maji na anachukua nafasi ya Mhandisi Anthony Sanga ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo.

Fadhili Mohamed Juma anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita Mkoani Geita naye kabla ya uteuzi huo, alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Lindi na anachukua nafasi ya Josephat Paulo Maganga ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma na kwamba Josephat Paulo Maganga anachukua nafasi ya Patrobas Katambi.

"Wateule wote wanatakiwa kuwepo Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Julai, 2020 saa 4:00 asubuhia', taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, imesema.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana