Featured

    Featured Posts

SERIKALI YAKOSA KARIBU SH. BILIONI 125 KWA WANANCHI ZAIDI YA 900,000 KUTOMILIKISHWA ARDHI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akikata utepe kuashiria kuzinduliwa rasmi ofisi ya ardhi mkoa wa Shinyanga jana. Wa pili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Taleck na wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimkabidhi Hati miliki ya ardhi Afisa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga wakati  wa uzinduzi ofisi za ardhi mkoa wa Shinyanga ambapo alizitaka taasisi za serikali kuhakikisha zinapima maeneo yao na kumilikishwa. Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Taleck.

Na Munir Shemweta, WANMM, SHINYANGA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema Serikali imekosa zaidi ya Sh, bilioni 125 kutoka kwa wananchi 900,000 nchini kutokana na kutomilikishwa ardhi na kupatiwa hati na kuwataka wale ambao viwanja vyao vimeshapimwa na michoro yake kupatiwa hati  waende ofisi za ardhi katika Halmashauri za wilaya kufuatilia hati ili waweze kumilikishwa ndani ya siku tisini.

Waziri Lukuvi ameagiza kuwa wamiliki wote nchini wakiwemo zaidi ya 60,000 wa mkoa wa Shinyanga ambao viwanja vyao vimepimwa na michoro yake kuidhinishwa wasipoenda ofisi za ardhi katika Halmashauri za wilaya kufuatilia hati ili waweze kumilikishwa ndani ya siku 90 kila mmoja atapelekewa stakabadhi ya malipo inayomtaka alipe kuanzia pale kiwanja chake kipopimwa na michoro kuidhinisha.

Waziri Lukuvi alisema hayo jana mkoani Shinyanga wakati wa uzinduzi ofisi za ardhi za mkoa huo ikiwa ni mfululizo wa uzinduzi wa ofisi za ardhi katika mikoa mbalimbali nchini.

"wale wamiliki ambao watashindwa kufuatilia hati katika kipindi cha siku tisini wataanza kudaiwa kodi ya pango la ardhi kuanzia pale michoro ilipoidhinishwa hata kama michoro hiyo iliidhinishwa mwaka 1962  ataanza kudaiwa kuanzia hapo maana itakuwa ni uzembe wake" alisema Lukuvi

Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi, serikali inataka kila Mtanzania apate hati miliki ya ardhi kwa mujibu wa sheria kwa kuwa serikali inashindwa kukusanya kodi ya ardhi kwa mtu ambaye hana hati na kuwataka wamiliki wachukue hati zao ili serikali ipate mapato na kutoa huduma katika sekta mbalimbali kama vile barabara, maji na hospitali.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack alishukuru kuanzishwa ofisi ya ardhi mkoa wa shinyanga na kueleza kuwa tayari amenza kuaona matunda ya ofisi hiyo kwa kupungua kwa migogoro ya ardhi katika mkoa wake na kuwahimiza wananchi wake kwenda katika ofisi za ardhi mkoa kuchukua hati.

"Kama mkoa tutahakikisha tunaleta utulivu kutokana na kuanzishwa ofisi za ardhi katika mkoa wa shinyanga kwa kuwa migogoro itakuwa imepungua", alisema Zainab

Tayari uzinduzi ofisi za ardhi katika mikoa mbalimbali limefanyika katika mikoa kumi na linaendelea katika mikoa ya Mara, Geita, Kagera, Lindi na Ruvuma.

Katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi Lukuvi aliwakabidhi hati za ardhi wananchi pamoja na taasisi za serikali zilizopo mkoa wa Shinyanga akiwemo Bibi wa miaka 77 Zainab Kechuba aliyeonesha furaha kubwa baada ya kukabidhiwa hati yake.

 Bibi Zainab alieleza kuwa, aliihangaikia hati yake kwa muda mrefu lakini sasa amefurahi kwa kupatiwa hati yake na kumuombea Rais John Pombe Magufuli umri mrefu na kuendelea kutawala Tanzania.

Waziri wa Ardhi alisema mwaka huu uwe mwisho wa migogoro ya ardhi kwa kuwa huduma za ardhi zimepelekwa karibu na wananchi kwa kuanzisha ofisi za ardhi za mikoa zenye wataalamu wa fani zote za ardhi sambamba na kusambaza vifaa mbalimbali vikiwemo vya upimaji katika mikoa.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana