CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani kimewaonya wanachama wake ambao hawakuongoza kwenye mchakato wa kura za maoni nafasi za Ubunge na Udiwani, waliokwenda kulalamika kwenye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani hapa.
Wanachama hao ambao walikwenda kwenye taasisi hiyo kulalamika kuwa wana-CCM wenzao ambao wameongoza kwenye kinyanganyiro hicho kwamba wametumia njia isiyosahihi ya kuongoza katika zoezi hilo, hali inayoendelea kuwaletea usumbufu wenzao kitendo ambacho chama inakikemea vikali.
Mwenyekiti wa chama hicho wilayani hapa Abdul Sharifu ametoa rai hiyo wakati akifungua mkutano Mkutano wa Uchaguzi kura za maoni za Jumuia ya wanawake UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa Chuo Cha Sanaa (TASUBA) wilayani hapa ambapo alisema kuna baadhi ya wanachama wake wamekweenda kulalamika wakidai walioongoza kwenye michakato hiyo wametumia njia isiyorasmi.
Ndani ya chama chetu kuna Kamati ya Maadili inayoshughulika na kero na malalamiko ya wana-CCM, hivyo ni vyema kupeleka malalamiko yao kwenye Kamati hiyo, badala ya kukiweka chama kwenye wakati mgumu kwa matatizo yanayiweza kushughulikiwa ndani ya chama, ukizingatia tunaelekea katika uchaguzi mkuu ambapo chama kitaenda kujinadi kwa wanachi, alisema Sharifu.
kuliko kwenda nje ya amepokea taarifa kwamba kuna wana-CCM walioongoza chaguzi za kura za maoni za ndani ya chama zilizomalizika kwa sasa wanahojiwa na taasisi hiyo.
Alisema kuwa chama kinatambua na kuheshimu sana majukumu yanayofanywa na taasisi hiyo ya Kiserikali, huku akiwaomba wanachama wanaolalamikiwa kujihusisha na kutoa au kupokea rushwa baada ya zoezi hilo ni vyema wakawarejesha kwenye chama, ili Kamati zinazohusika na maadili ziweze kuchukua hatua kwa wanachama husika.
Chama kinasikitishwa na baadhi ya wanachama ambao wanakwenda TAKUKURU kupeleka malalamiko baada ya kumalizika kwa chaguzi, hatua hii inaweza kuiweka pabaya chama chetu wakati huu tunaelekea kwenye uchaguzi Mkuu mwishoni mwa mwaka huu, niwaombe wenzetu ambao wanatekeleza Ilani ya chama chetu, kuwapuuza wanaokwenda kulalamika baada ya kumalizika, kwanini wasitoe taarifa zao kabla ya uchaguzi, alisema Sharifu.
Post a Comment