Angelina Mabula sasa haliwezi kuwa jina geni tena miongoni mwa mamilioni ya Watanzania na kwingineko Duniani.
Ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambaye kwa aliyefuatilia kwa karibu utendaji kazi wake, atakubali kwamba ni mwanamke mchapakazi ambaye amefanikiwa kulifanya jimbo hilo kunawiri kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na zamani.
Pamoja na jimbo hili kujipatia Mbunge Mwanamke ambaye ni mchapakazi, lakini limebahatika pia kuwa miongoni mwa majimbo ambayo yana kiongozi mwenye hadhi ya Naibu Waziri, maana Angela Mabula pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye hakika ameweza kuendana na kasi ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli.
Angela amefanya mengi sana ya kupigiwa mfano katika Kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, na kama ilivyo ada, Wabunge wote ambao ni wa CCM hutayarisha Taarifa zao za Utekelezaaji wao wa Ilani ya CCM jimboni na kuiwasilisha Makao Makuu ya CCM.
Kwa kuwa Blog hii ya Taifa ya CCM imebahatika kuipata taarifa hiyo ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Mheshimiwa Angela Mabula ya kipindi cha Oktoba 2015 hadi Juni 2020, tumeichapisha ili na wewe mdau uweze kuisoma taarifa hiyo, hatua kwa hatua. Kuisoma...BOFYA HAPA
Post a Comment