TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM YA MBUNGE WA JIMBO LA SINGIDA KASKAZINI (2018-2020) MH. ENG. JUSTIN MONKO
Mh. Eng. Justin J. Momko Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini (2018 - 2020)
Mh. Eng. Justin J. Momko Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini (2018 - 2020) alipokuwa akiapishwa Bungeni mwaka 2018.
1.0 UTANGULIZI:
Utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) huanza pale tu kiongozi mwenye dhamana anapokabidhiwa jukumu la utekelezaji. Kama inavyoelezwa kwenye Katiba ya CCM ya mwaka 1977 Toleo la mwaka 2012, Sehemu ya Kwanza ibara ya 5 (7) kwamba, “Kusimamia haki na maendeleo ya Wakulima, wafanyakazi na wananchi wengine wenye shughuli halali za kujitegemea; na hasa kila mtu ana haki ya kupata malipo yanayostahili kutokana na kazi yake”
Hivyo kwa mwongozo huo, ifuatayo ni taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha mwaka 2018 hadi 2020 kama ilivyoandaliwa na Mh. Eng. Justin J. Momko Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini (2018 - 2020)
Taarifa hii imegawanyika katika sehemu mbalimbali kama ilivyoanza Utangulizi, Shukrani na kiini cha taarifa ambacho kinaeleza utekelezaji uliofanyika kwa ujumla katika Nyanja mbalimbali kijamii, kisiasa na kiuchumi. Taarifa hii imeeleza vitu vingi ikiwemo mafanikio katika sekta ya Afya, uchumi,
miundombinu yote na mengineyo (mfano: ahadi zilizotekelezwa na Mh. Mbunge pamoja na ziara mbalimbali
na kuelezea changamoto zilizopo na mwisho kabisa ni Hitimisho.
1.1 Shukrani
Kwa heshima na taadhima nawasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kipindi cha Mwaka 2018 hadi 2020 Jimbo la Singida Kaskazini Mkoa wa Singida.
Ninayo heshima kubwa kuwashukuru viongozi wangu wa CCM Taifa, Mkoa, Wilaya na gazi ya Kata na Mashina.
Ninajiona mwenye furaha sana kuona wamenipa ushirikiano wa kutosha ninapotekeleza majukumu yangu na harakati nzima ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), na tena kwa kasi. Ninaahidi kuendelea kutekeleza Ilani ya Chama chetu kwa ufanisi mkubwa Zaidi kama Chama kitanipa tena ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hili katika mhula mwingine.
Napenda kuwashukuru viongozi wote wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Singida DC, kwa ushirikiano walioonyesha katika kuitekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM tangu nilipoingia madarakani mwaka 2018 hadi sasa 2020
Kwa moyo wa dhati kabisa nipende kuwashukuru viongozi wa Dini wa Jimbo la Singida Kaskazini kwa kuendelea kuliombea Jimbo letu na Taifa letu kwa sala, dua na maombi. Kwa ujumla kupitia dua na sala tunaendelea kuwa na afya njema na Amani na kuendelea kulitumikia Taifa letu.
Shukrani nyingi zimwendee Mhe. Mkuu wa Wilaya na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama, pamoja na watumishi wote na Serikali na wananchi wote kwa kazi nzuri wanayoifanya. siyo rahisi kumtaja mmoja mmoja kwenye taarifa hii lakini kwa ujumla, ninawashukuru wadau wote waliochangia kwa hali na
mali ili kupatikana kwa mafanikio makubwa kwa kipindi kifupi cha miaka hii miwili niliopewa dhamana kuongoza,
Nawaomba wadau wote tuendelee kushirikiana kwani umoja ni nguvu na ushindi wetu.
Post a Comment