Featured

    Featured Posts

TAASISI ZATAKIWA KUJIENDESHA ZENYEWE LICHA YA JANGA LA CORONA

Arusha, Tanzania
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imezitaka Taasisi zote zilizopo chini ya Wizara hiyo kufanya kazi kwa ubunifu na kufanya uwekezaji wenye tija ili kuhakikisha zinajiendesha zenyewe na kuipunguzia Serikali kuu mzigo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameyasema hayo alipofanya ziara katika maeneo mbalimbali ya uwekezaji yanayomilikiwa na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha AICC na kuwataka watendaji wake kuwa wabunifu.

Amezitaka taasisi hizo kuhakikisha zinajiendesha kwa ubunifu na kuondokana na zana kuwa Serikali itazisaidia kujiendesha kwa kisingizio cha uwepo wa janga la Corona.

Nae Mkurugenzi mwendeshaji wa kituo hicho cha kimataifa cha mikutano cha Arusha Bw. Elishilia Kaaya amesema taasisi hiyo imeyapokea maagizo hayo ya serikali na kwamba changamoto kubwa iliyopo mbele yao licha ya kuathirika na janga la corona ni kuhakikisha inajiendesha bila ya kutegemea ruzuku kutoka serikalini.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana