Featured

    Featured Posts

TAKUKURU TEMEKE YAOKOA MAMILIONI YA FEDHA.

Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa Temeke Ramadhan Ndwatah akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo.
…………………………………………………………..Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Temeke imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi milioni 79, 540, 500 kutokana na kufanya uchunguzi sehemu mbalimbali ikiwemo fedha za SACOSS, Mfuko wa Jimbo pamoja na risiti zilizoghushiwa. 
 fedha hizo zimeokolewa katika kipindi cha cha mwezi April hadi Juni mwaka huu wakati TAKUKURU ikiendelea na majukumu yake ya kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa mujibu wa sheria namba 11 ya mwaka 2007.
 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa Temeke Ramadhan Ndwatah, amesema kuwa wakati wanatekeleza majukumu wamepokea taarifa 103 zinazohusu vitendo vya rushwa.
 Ndwatah ameeleza kuwa katika kipindi hicho Manispaa ya Temeke pamoja na taasisi binafsi zinaongoza kwa kulalamikiwa na kufanikiwa kufunguliwa majalada mapya ya uchunguzi yaliyofunguliwa na kufikia hatua za uchunguzi wa kina yapo 15, huku majalada mengine yanaendelea na uchunguzi katika hatua mbalimbali.
 Amefafanua kuwa katika kesi ya kwanza inamhusu Bw. Elias Mtarawanje ni Diwani wa Kata ya Kijichi ambaye alifikishwa mahakamani kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya Sh. 1,000,000 ili amsaidie mtu aliyetakiwa kulipwa fidia ya kiwanja, kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.
 Kesi ya pili Bw. Ally Mtiga ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Tambukareli alifikishwa mahakamani kwa kosa la kujipatia fedha kwa njia ya utanganyifu kwa mwananchi ili aweze kumsaidia kupata leseni ya makazi.
 kesi ya tatu Sophia Milanzi ni Afisa Mtendaji Mtaa wa Kizinga alifikishwa Mahakamani kwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh. 50,000 kutoka kwa mwananchi ili ampatie huduma ya kubadili jina kwenye rejesta ya makazi.
 Kesi ya nne Moris Sendi ni Afisa Mtendaji Mtaa wa Rangi Tatu alifikishwa mahakamani kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa Sh. 70,000 kwa ajili ya kumsaidia mwananchi aendelee kufanya biashara eneo la Rangitatu.
 “TAKUKURU inaendelea na kujumu la kuelimisha umma kupitia njia mbalimbali, lengo ni kuhakikisha wananchi wanashiriki kwa vitendo katika mapambano dhidi ya rishwa” amesema Bw. Ndwatah.
 Katika hatua nyengine Bw. Ndwatah amesema kuwa katika kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu, wamejipanga kwa kuendelea kuelimisha umma kupitia njia mbalimbali ikiwemo kufanya mikutano ya hadhara, semina kwa wagombea pamoja mawakala ili kudhibiti vitendo vya rushwa katika kipindi cha uchaguzi.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana