Featured

    Featured Posts

TBS YATOA MAFUNZO KWA WAJASILIAMALI KAGERA.

Mkuuwa wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro akikagua bidhaa za wajasiliamali walizozileta kama mfano mara baada ya kuzindua mafunzo yaliyotolewa na wawezeshaji wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa wajasiliamali wa mkoa wa Kagera, leo
Na Mwandishi wetu, Bukoba.
Shirika la viwango Tanzania TBS limeendesha mafunzo
maalumu ya ujasiliamali na umuhimu wa ubora wa bidhaa
kwa wajasiliamali mkoani Kagera kwa lengo la kuboresha
bidhaa zao ili kuendana na ushindani wa soko la dunia.

Mafunzo hayo yamefanyika julai 27,mwaka huu katika
ukumbi wa Bukoba hotel ambayo yamewahusisha 
wajasiliamali Zaidi ya 50 kutoka wilaya za mkoa huo
ambapo wajasiliamali hao wameelezwa umuhimu wa kuwa na
alama ya ubora(TBS)  kwenye bidhaa zao.

Akifungua mafunzo hayo ya siku moja mkuu wa wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro amelishukuru shirika hilo kwa kuamua kuwafikia wajasiliamali kwenye maeneo yao na kuweza kuzijua changamoto zao katika usindikaji wa bidhaa zao.

Kinawiro amesema kuwa wajasiliamali ni watu muhimu katika
ukuaji wa uchumi wa taifa ambao wanatakiwa kusaidiwa kwa
kupewa elimu ya ujasiliamali pamoja na namna bora ya
utunzaji wa bidhaa tangu zikiwa malighafi hadi kufikia hatua ya
kwenda sokoni.

“Wajasiliamali ni watu muhimu kwa taifa letu, TBS mnalo
jukumu kubwa sana la kuhakikisha wadau hawa wanapata 
elimu sahihi na bora yenye lengo la kuwainua katika shughuli 
zao, tunaona sasa nchi yetu imefikia uchumi wa kati mchango wa watu hawa upo mkubwa.” Ameeleza Kinawiro.

Ameongeza kuwa mkoa wa Kagera unapakana na nchi 
takribani nne ambazo zinaweza kuwa fursa kwa wajasiliamali 
wa mkoa huo hivyo wajasiliamali wakikosa alama za ubora 
kwenye bidhaa zao watakosa masoko kwenye nchi hizo 
kwakuwa zitakuwa hata hazitambuliki hata kama ni nzuri.

Aidha Kinawiro amewataka SIDO na TBS kuwasaidia 
wajasiliamali kupata vifungashio bora ili kuweza kuuza bidhaa
 zao kwa usafi na ubora na pia waweze kupata faida ambapo
amesema kuwa changamoto hiyo imekuwa kero na kuwafanya wajasiliamali kutumia vifungashio vivyobora na kuwapelekea walaji kushindwa kununua bidhaa zao.

Hamisi Sudi ni meneja utafiti na mafunzo kutoka TBS akiongea
kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa shirika hilo amesema kuwa
wamekuwa wakitoa mafunzo hayo mara kawa mara kwa 
wajasiliamali nchini lengo ni kuwawwezesha kuzalisha bidhaa 
zenye ushindani kwenye soko la dunia.

Ameeleza kuwa shirika hilo linaendelea kupambana ili 
kuhakikisha wajasiliamali wote nchini wanakuwa na alama za 
ubora (TBS) kwenye bidhaa zao ili kumridhisha mlaji wa 
mwisho kuiamini bidhaa hiyo kutokana na uwepo wa alama 
hiyo.

Bw.Sudi ameongeza kuwa zipo changamoto kwa wajasiliamali 
wanaoshindwa kukidhi vigezo vya kuweza kupewa alama na 
badala yake wanapeleka bidhaa zao sokoni huku wakijua 
hazina ubora uliothibitiwa na mamlaka husika ambalo suala 
hilo huwapelekea kukosa masoko ya ndani nan je ya nchi kwa
 ujumla.

Amewataka wajasiliamali kuwa na tabia ya kuhudhuria 
mafunzo mbalimbali yanayotolewa na shirika hilo ili kuweza 
kuwajengea uwezo binafsi wa kuzalisha bidhaa zilizo bora na 
kuweza kupata masoko makubwa nay a kuaminika.

Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wajasiliamali 
waliohudhuria mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo 
waliyoyapata yatawasaidia kuanza kuzalisha bidhaa zenye 
ubora Zaidi na kuweza kupata masoko makubwa.

Matungwa Daniel ni mkurugenzi wa kiwanda cha Nyaka 
Food kilichopo Manispaa ya Bukoba ambaye amesema kuwa 
amekuwa akipata changamoto ya kuuza bidhaa zake nje ya 
nchi kutokana na bidhaa zake kutokuwa na alama ya ubora 
(TBS) suala linalompelekea kukosa masoko licha ya kuwa 
watu kutoka nchi za nje wanazipenda bidhaa zake.

Ameongeza kuwa serikali ikiwasaidia wajasiliamali hao kupata alama ya ubora kwa haraka itawasaidia kupata masoko na kupunguza usumbufu kwao pale wanapokwenda kuuza bidhaa hizo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana