Baadhi ya wakulima wa zao la kahawa wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera wameomba Serikali kupitia bodi ya Kahawa kuwachunguza na kuwachukulia hatua baadhi ya wanunuzi wa zao hilo na wanaotoa vitishio kwa wakulima kwamba, wasiuze kahawa yao kwa wanunuzi wengine kuwa watu wa aina hiyo wanakiuka agizo la Serikali linalotaka mkulima kuuza kahawa yake kwa mnunuzi yoyote mwenye bei nzuri.
Abdutwahibu Hassan na Selestine Mbatina ni baadhi ya wakulima wa kata ya Nkwenda Wilayani humo ambao walitoa malalamiko yao mbele ya mkurugenzi wa bodi ya kahawa nchini TCB, Uongozi wa tume ya ushindani nchini na uongozi wa mkoa wa Kagera katika mkutano wa wakulima wa zao hilo,viongozi wa Amcos na makalani wa vyama vya ushirika.
Hassani alieleza kuwa wao kama wakulima wamewekeza sana katika chama chao kikuu cha ushirika cha Karagwe KDCU tangu kianzishwe lakini hawawatendewi kama walivyopanga na kujadili na wakulima mwishowe wanatendewa kinyume na makubaliano hivyo wameamua kutouza kahwa yao na kubaki nayo ndani.
“KCDU ni chama chetu hawatutendei haki wajirekebishe walitangaza kununua kahawa kwa bei ya shilingi 1,200 kwa kila kilo lakini wamenunua kwa shilingi 1000 hiyo 200 yetu iko wapi?na bado wanakuja wanataka tuwauzie kahawa nyingine kupitia Amcos zetu hii si haki pia, tunapata vitisho kutoka kwa baadhi ya viongozi ambao hatuwataji hapa ila akija baba yetu Rais Magufuli tutamwambia tutawataja ”aliongea huku akibubujikwa na machozi Hassani.
Naye Mbatina alisema amejihusisha na kilimo cha kahawa hivi sasa ni mwaka wa 40,akaelekeza malalamiko yake kwa TCB kwamba washughulikie haraka sula la baadhi ya viongozi wa vyama wanaowatisha wakulima hao pale wanapouza kahawa yao kwa wanunuzi wengine ili nao waweze kunufaika na zao lao.
“Tulitangaziwa bei kuwa 1,300 ikaja 1,200 lakini malipo yetu yanakuja tofauti pale tunapokwenda kuuza kwenye ushirika basi bodi kama nyie mmeishajua tatizo liko wapi litafutie ufumbuzi msituchanganye wakulima”alieleza mzee Mbatina .
Oscar Domini ni meneja wa KDCU alipohojiwa na uhuru kwa njia ya simu alisema kuwa watu wanaosema wanatishwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika ikiwemo KDCU ni waongo na wazushi kama ni kweli vyombo vya ulinzi na usalama vipo wachukue hatua.
Sisi hatununui kahawa kutoka kwa kulima,sisi kama ushirika tunaowajibu wa kusimamia vyama vya msingi katika kukusanya kahawa hatununui kwa mtu mmoja mmoja hata wanunuzi wengine wenye leseni wanaruhusiwa kununua sisi hatuna ugomvi na mtu huo ni uzushi”alileza Dominic
Daniel Damiani na Harbert Katagila ni wa nunuzi binafsi walimuleza mkurugenzi wa TCB nchini kuwa wanazo pesa tiyali kwa ajili ya kununua kahawa baada ya agizo la Serikali kutolewa kuwa mnunuzi yoyote mwenye fedha anaruhusiwa kununua kwa kufcuata taratibu lakini walikuwa memekwama, katika suala zima la kupata leseni kwa kuelezwa na marajisi wa vyama vya ushirika nchini kuwa mikataba yao inamapungufu.
“Tunashukuru Serikali kwa kutupa nafasi hii ya kila mwenye bei nzuri ende kwenye Amcos au Chama cha msingi aweke mkata nao anunue kahawa ni vizuri tumeletewa mfano wa mkataba tutakaotumia nchi nzima mbapo utaondoa changamoto za awali je tukiisha kamilisha na tukapata leseni kahawa tutaipata wapi? Wakati wenzetu vyama vya suhirika wameishakusanya yote tena kwa mkopo wanawaacha
wananchi wanalia,hiyo furaha wataipata wapi? na muda wa msimu kuisha unakaribia “alieleza Damiani.
Baada ya vikao hivyo viwili vilivyofanyika kwa nyati tofauti vikishirikisha bodi ya kahawa nchini,tume ya ushindani nchini na uongozi wa mkoa,pia kushirikisha wakulima wa kahawa na viongozi wa Amcos Wilayani Kyerwa viongozi hao walitia majibu na msimamo wa Serikali.
Naye afisa uchunguzi kutoka tume ya ushindani Waubile Malata aliwataka wanunuzi ambao ni wakubwa vikiwemo vyama vikuu vya ushirika kutowatisha na kuwadidimiza wanunuzi wadogo wanaochipukia kwani hilo siyo lengo la Serikali.
“Hata kama unamisuri mikubwa usiitumie kuwanyanya wale wanaochipukia hiyo itasaidia kukuza uchumi wa kila mmoja wetu na kufikia kile tunachokilenga”alieleza Malata.
Naye mkurugenzi wa TCB nchini Prof. Jamal Adam alisema kuwa Serikali kupitia bodi imesema hakuna mnunuzi yoyote binafsi anayezuiwa kununua kahawa ili mradi afuate sheria na taratibu ikiwemo kuwa na leseni na bei inayompa furaha na inayomnufaisha mkulima na kumpa furaja.
“Tumeishapata taarifa kuwa watu wanatishwa nawashauri wale wanaofanya hivyo waache mara moja wasiwachanganye wakulima nawaomba wakulima fuateni mwongozo wa Serikali unavyosema kahawa ni
yako ulipanda,ukapalilia,ukavuna,ukaanika sisi hatukuwepo tunapofikia wakati wa kuuza tunakuja eti tunakupangia uuze wapi haiwezekani mhe:Rais wa Magufuli ameishaagiza wanunuzi wenye fedha na bei nzuri waje na kununue kahawa”alisema Pfor. Adam
Alisema ukiangalia watu wanaohusika na kahawa kuanzia bodi mpaka wanunuzi wote wamenawili lakini mkulima hana furaha amechoka wakati ndio mwenye mali hivyo Serikali imekuja na kauli mbiu kuwa sasa kahawa ni furaha kwa mkulima na furaha hiyo italetwa na wanunuzi wanapokuja na bei nzuri ya kulidhisha.
Mwanzoni mwa mwezi huu wakati waufunguzi wa msimu mpya wa ununuzi wa kahawa 2020 mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti alisema kuwa anahitaji wanunuzi wenye fedha na siyo manenomane ili wananchi waweze kunufaika na zao hilo na pia mnunuzi akinunua kahawa ya mkulima alipe fedha ndani ya masaa 48 la sivyo asichukue kahawa hiyo.
Post a Comment