*********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Wananchi wameungana na viongozi mbalimbali wa nchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli katika misa ya kumuaga Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Hayati Benjamin Wiliam Mkapa katika uwaja wa Uhuru JIjini Dar es Salaam.
Hata hivyo taarifa iliyotolewa na Mwanafamilia wakati wa Misa ya kumuaga Rais Mstaafu Hayati Benjamin William Mkapa imesema Sababu ya kifo chake ni Mshituko wa Moyo.
Akizungumza katika misa hiyo Msemaji wa Familia Bw.William Erio amesema kuwa mzee wetu alikuwa hajisikii vizuri akaamua kwenda hospitali na baada ya vipimo alionekana kuwa ana ugonjwa wa Maralia hivyo akalazwa kwa siku hiyo na Alhamisi mchana aliendelea vizuri na baadae usiku alipatwa na mshtuko akafariki dunia ikisemekana chanzo cha kifo chake ni Ugonjwa wa Moyo.
“Alikuwa anasikiliza taarifa ya habari na baadae alitaka kuinuka kukaa akainamisha kichwa na hiyo mpaka walipokuja kumpima akawa amethibitika kwamba amefariki, sababu yake ya kifo alipata mshituko wa moyo”. Amesema Bw.Erio.
Post a Comment