…………………………………………………………………………………..
Timu ya Yanga imetinga nusu fainali ya Michuano ya Kombe la shirikisho Azam Sport Federation kwa kuichapa mabao 2-1 Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera Michezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga imelipa kisasi cha kufungwa mabao 3-0 na Kagera Sugar mechi ya Ligi Kuu iliyopigwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Kagera walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa kiungo wao hatari Awesu Awesu dakika ya 19 kwa shuti kali lililomuacha mlinga mlango wa Yanga baada ya kupokea mpira kutoka kwa Yusuph Mhilu.
Hadi timu zinaenda mapumziko Kagera Sugar walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote mbili kufanya mabadiliko huku Yanga wakinufaika zaidi kunako dakika ya 51 David Molinga aliwanyanyua mashabiki wake kwa kupachika bao kwa kichwa akimalizia pasi ya Mrisho Ngassa.
Yanga walipata bao la pili kupitia kwa Deus Kaseke kwa njia ya Penalti baada ya Mrisho Ngassa kuchezewa faulo na Juma Nyosso ndani ya kumi na 18 na mwamuzi kuamua iwe Penalti.
Kagera Sugar walipata pigo dakika ya 78 baada ya Awesu Awesu kuonyeshwa kadi nyekundu kutokana na kuwa na kadi za njano mbili.
Kwa ushindi huo Yanga wametinga nusu Fainali kwa mara ya tano na sasa wanamsubiri mshindi kati ya Simba na Azam FC Mchezo utakaopigwa kesho uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Nayo Namungo FC nao wametinga nusu fainali ya michuano hiyo kwa kuichapa mabao 2-0 timu ya Alliance huku wakimsubiri mshindi kati ya All Stars ya Tanga au Ndanda FC kutoka Mtwara mchezo utapigwa katika uwanja wa Mkwakwani jijni Tanga.
Post a Comment