Featured

    Featured Posts

DC MTWARA: WANANCHI CHANGAMKIENI FULSA YA MATUMIZI YA GESI ASILI MAJUMBANI KWENU

Na Faruku Ngonyani, Mtwara.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya hiyo kuchangamkia fursa ya kuwepo kwa Gesi asilia ya matumizi majumbani.

Ametoa wito huo alipotembelea mtambo wa kupunguza mgandamizo wa gesi asilia kwa matumizi ya majumbani uliyojengwa eneo la Banadari kata ya Reli Manispaa Mtwara Mikindani ambapo mtambo huo unauwezo wa kuanganisha matumizi ya gesi asili kwa nyumba 1000.

Ujenzi wa Mtambo huo umejengwa na Shirika la Maendeleo la Petrol Tanzania (TPDC) ukiwa na lengo lakupunguza mgandamizo (pressure) ya  gesi inayosafirishwa kwa njia ya mabomba kwenda kwenye matumizi ya majumbani.

Injinia wa TPDC Eva Swala ameongeza kuwa gesi haiwezi kwenda majumbani kwa matumizi moja kwa moja lazima ipite kwenye mtambo huo ili iweze kupunguza mgandamizo utakaoendana na matumizi yao.

Aidha Injinia huyo ameongeza kuwa kwa Mkoa wa Mtwara kuna jumla ya Vituo vitatu (3) vya kupunguza mgandamizo wa gesi asilia  majumbani, ambapo amevitaja vituo hvyo ni pamoja na kituo cha Mtwara Ufundi,kituo cha Lilungu na kituo cha bandari ambapo kwa ujumla vituo vyote  vinauwezo wa kuhudumia nyumba elfu tatu (3000).

Gharama ya majumbani Unit Moja ya gesi hiyo intozwa shilingi elfu moja (1000) ambapo unaweza kuitumia kwa siku mbili kwa matumizi ya kawaida.

Lakini Mkuu wa Wilaya ya Mtwara ameawsisitiza Shirika la maendeleo la petrol (TPDC) kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kuhamasika zaidi juu ya matumzi ya Gesi asilia majumbani.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana