Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dodoma baada ya shule za serikali kuibuka kidedea katika matkeo ya kidato cha sita 2020.
Baadhi ya Wataalamu wa Elimu TAMISEMI wakimfatilia kwa makini Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo(hayupo pichani) wakati akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dodoma.
……………………………………………………..
Na. Alex Sonna, Ddoma
Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Magufuli ndio siri iliyopelekea shule nane za serikali kuingia kwenye kumi bora katika ufaulu wa matokeo ya kidato cha sita 2020 kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika sekta ya elimu.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo wakati akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dodoma.
Aidha Mhe. Jafo amesema kuwa ufaulu huo ni matinda mazuri yaliopandwa na serikali katika Sekta ya Elimu ambapo kwenye matokeo yaliyotangazwa ufaulu umeongezeka kwa wanafunzi wa kidato cha sita kutoka asilimia 98 kwa mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 99.51 kwa mwaka.
“ katika matokeo hayo shule za Serikali nane zimeweza kuingia katika shule kumi bora kwa mara ya kwanza zikiwemo shule za kata 3 ambazo ni Kasimiri, Mwandeti na Dareda,” ameeleza Mhe. Jafo.
Mhe. Jafo amesema kuwa shule za Serikali zilizoshika nafasi kumi bora kuwa ni Mzumbe, Shule ya wasichana Tabora, shule ya wavulana Tabora, Iiliboru na Kibaha .
“wazazi walikuwa hawapendi kuwapeleka watoto wao kusoma katika shule za serikali wanapochaguliwa kujiunga na shule hizo, hivi sasa shule hizi zinafanya vizuri na kuwa na ufaulu mkubwa wa kuwa tegemeo kwa wazazi kuwapeleka watoto wao” amesisitiza Mhe. Jafo
Pia Mhe. Jafo amesema kuwa anawapongeza Wanafunzi wote wa kidato cha Sita kwa kusoma kwa bidi na kupata ufaulu mzuri japokuwa kulikuwa na changamoto ya ugonjwa wa CORONA nchi ya Tanzania bado waliweka juhudu katika masomo na kufaulu mitihani yao vizuri.
“Bila kusahau nawashukuru walimu waliojitolea kufundisha kipindi hicho cha changamoto ya Corona na kuhakikisha shule zetu zinapata ufaulu huu”, amewashukuru Mhe. Jafo.
Kwa kutamatisha Mhe. Jafo amesema kuwa Serikali imetumia kiasi cha shilingi trilioni 1.09 katika utoaji wa elimu bila malipo ambayo imehamasisha sekta ya Elimu nchini, pia kiasi cha shilingi milioni 588 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu jambo hili limesaidia kuongeza idadi ya ufaulu wa wanafunzi nchini.
Post a Comment