Featured

    Featured Posts

MGOMBEA UDIWANI KATA YA KUNDUCHI KWA TIKETI YA CCM AREJESHA FOMU NEC


Diwani wa Kunduchi, Dar es Salaam aliyemaliza muda wake ndugu Urio, akirejesha fomu ya kuwania tena udiwani wa Kata hiyo kwenye kwenye ofisi ya Kata ya Kunduchi, jana.

Mgombea huyo alisindikizwa na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  kwenye Ofisi hiyo.


Akizungumza  baada ya kurudisha fomu hiyo aliwashukuru wakazi wa Kata hiyo ya Kinduchi kwa kumuamini kipindi cha miaka mitano iliyopita na kuahidi kufanya kazi kwa bidii zaidi kama watampatia miaka mingine mitao tena.

Aliwaomba wanachama  kuhakikisha wanawapa 'utatu mtakatifu' kwa kuhakikisha wanatoa kura nyingi kwake, Mgombea Ubunge jimbo la Kawe Askofu Gwajima na Urais kwa Jemedari Rais Dk. John Magufuli.


Baada ya kukamilisha kurudisha fomu wafuasi wa CCM waliungana kwa misafara ya mapikipiki na magari kuelekea jimboni Kawe kuongeza nguvu kwenye msafara wa mgombea Ubune wa Kawe ambaye pia alikuwa anarejesha fomu Wilayani Kinonfoni.


Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzu (NEC), kampeni za Uchaguxi Mkuu utakaofanyika Siku ya Jumatano, Oktoba 28, zinaanza rasmi Agosti 26, 2020 hadi Oktoba 27, 2020.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana