Featured

    Featured Posts

MKAA MWEUPE WAPOKELEWA NA WANANCHI KWA MOYO MWEUPE

Ofisa Mauzo Ezekiel Kwaka (kulia), akitoa maelezo kuhusu ubora wa Mkaa Mweupe wakati wa Maonesho ya Wakulima ya Nanenane Kanda ya Kati kwenye viwanja vya  Nzuguni, jijini Dodoma yaliyomalizika hivi karibuni. Mkaa huo ambao ni rafiki wa mazingira ulikuwa unauzwa kwenye mifuko sh. 1000, 2000, 3000, 4000 na 5000 kutokana na wingi wa vipande vya mkaa.
Vipande vya Mkaa Mweupe vidogo na vikubwa ambapo vidogo hutumika kwa majiko madogo na vikubwa kwa majiko makubwa.
Aristotle Nikitas  Meneja Masoko wa Kampuni ya Premium Active Tanzania Limited, inayotengeneza  Mkaa Mweupe, akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Singida, Dk. Rehema Nchimbi baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi wa pili kundi la Wajasiriamali na Wawekezaji wadogo wakati wa kilele cha Maonesho ya Wakulima ya Nanenane Kanda ya Kati kwenye viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Ofisa Mauzo,  Ezekiel Kwaka akielezea kuhusu matumizi ya vipande vidogo vya mkaa ambapo alisema kati ya vipande vitatu au 4 vinaweza kupika vyakula kwa takribani masaa manne bila kuzimika. Mfuko mmoja wenye vipande vidogo kumi huuzwa sh.1000.
Mkaa Mweupe ambao hutengenezwa kwa kutumia majani maalumu, hautoi moshi ukiwashwa
 Jiko kubwa linalotumia vipande vikubwa vya Mkaa Mweupe ambalo lilikuwa linaoneshwa jinsi mkaa huo unavyoivisha kande. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana