Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
Uongozi wa Klabu ya Yanga umeendelea na msimamo wake wa kukata rufaa Shauri la Mchezaji Benard Morrison kwa madai bado ana mkataba na Klabu hiyo.
Hatua ya Yanga kukata rufaa katika mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) inakuja baada ya kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji ya TFF kuamuru Morrison ni mchezaji huru.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Yanga Dkt Mshindo Msolla amesema wanatambua kuwa Morrisin bado ana mkataba na Yanga unaoishia Julai 2022.
Amesema, Rufaa ya mchezaji Morrison kwenda mahakama ya CAS imekamilika na tayari imetumwa leo ili kuweza kupata kusikilizwa.
Msolla amsssma," leo tumetuma rufaa yetu CAS na tunatarajia suala hili litasikilizwa na kutolwa maamuzi ya haki kwa pande zote na kwa upendo wetu bado tunaamini ni mchezaji wetu,"
Amesisitiza kuwa, hukumu ya TFF imeonesha kuwa uwepo wa mkataba na imemuweka mchezaji huru hivyo tumeona tukatafute haki mbele kwa kuwa hapa kwetu wameshindwa kutenda haki inavyostahili.
Ikumbukwe kuwa Shauri la Morrison liliweza kuchukua siku tatu kabla ua kutolewa maamuzi na kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji kwa kumuweka huru Morrison na anaweza akasajiliwa na timu yoyote.
Morrison tayari ameshatambulishwa Na Klabu ya Simba kama mchezaji wao kwa mkataba wa miaka miwili na ameshacheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Vital O ya Burundi.
Post a Comment