Hatua ya kiongozi huyo mkuu wa Wakatoliki kuondoka kwenye makao makuu ya Vatican na kwenda kusali nje katika kipindi hiki cha vita dhidi ya korona, imechukuliwa na wafuasi wake kuwa ishara ya umuhimu wa suala la Beirut kwa Kanisa.
Papa huyo alishawaombea wahanga wa mkasa huo kwenye ibada ya asubuhi mbele ya hadhara yake, lakini ameongeza ibada nyengine maalum kwa Lebanon, katika siku ambayo Wakristo wanaamini Bikira Maria alimtokea Papa Liberius miaka 1,662 iliyopita.
Wageni na watalii walijipanga kwenye mitaa ya Rome kumkaribisha Papa Francis jana Jumatano.
Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, aliondoka makao makuu Vatican hapo jana na kusali kwenye kanisa la Basilica mjini Rome kwa ajili ya taifa la Lebanon, baada ya mripuko kwenye ghala la bandari kuuwa zaidi ya watu 135.
Post a Comment