Serikali kupitia wizara ya afya jinsia wazee na watoto imeokoa zaidi ya shilingi bilioni 700 kwa mwaka zilizokuwa zinatumika kutibu zaidi ya wananchi 500 wanaougua magonjwa mbalimbali nje ya nchi baada ya kujiongezea uwezo wa kutibu magonjwa mengi kwa asilimia 90 ambayo matibabu yake yalikuwa hayapatikani nchini.
Uokoaji huo wa fedha hizo kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel unatokana na Serikali ya awamu hii ya tano kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya ikiwemo kuwekeza katika mitambo ya kisasa ya kimatibabu.
Pamoja na kufikia asilimia 90 katika utoaji wa matibabu kwa magonjwa yaliyokuwa hayatibiwi nchini taarifa ya hospitali ya mkoa wa Manyara iliyosomwa na mganga mfawidhi Dkt. Catherine Magari imemueleza Naibu Waziri kuwepo uhitaji wa wataalam wa magonjwa mbalimbali hospitalini hapa hususan madaktari.
Post a Comment