MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesitisha leseni ya utoaji huduma za utangazaji wa kituo cha Clouds Televisheni na Redio kwa siku saba kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 3, mwaka huu.
Aidha TCRA imekitaka kituo hicho kuanzia muda wa agizo hilo mpaka mwisho wa siku ya leo kuahirisha matangazo yote na kutumia muda wote uliobakia wa siku ya leo kuomba radhi kwa umma wa Tanzania kwa kukiuka Kanuni za Utangazaji kupitia kipindi cha Clouds 360.
Post a Comment