Featured

    Featured Posts

WAZIRI LUKUVI AINGILIA KATI MGOGORO WA KIKONGWE NDESIO

 


………………………………………………………………

Na Ahmed Mahmoud Arusha

WAZIRI wa Ardhi nyumba na makazi ameombwa kuingilia kati mgogoro wa
ardhi uliodumu kwa miaka kumi kati ya Bi Angaza Selemani (85) na Elias
Barnabas Chami pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Mashaka Gambo.

Katika barua yenye kumbukumbu namba 01/M/D/RC/AR/2019 ya Novemba 23
2019 iliyoandikwa na Bi Angaza kwenda kwa William Lukuvi anamlalamikia
aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa manyanyaso anayoyapata toka
Gambo.

Barua hiyo ambyo Gazeti hili limefanikiwa kuona nakala yake Kikongwe
huyo anamlalamikia Gambo kwa kushindwa kumsaidia katika mgogoro wake
na mtoto wa aliyekuwa mpenzi wake.

Katika barua hiyo Bi Angaza anamtuhumu Gambo kwa kumtapeli Tsh
2,000,000 zilizokuwa katika akaunti yake Benki ya NBC na alipofika
benki kutaka kutoa fedha zake hakukut kitu jmbo ambalo linamtia
mashaka kuwa Gambo ndio alimpa namba ya akaunti yake hivyo kukosekana
kwa fedha hizo

Jambo hilo linampa mashaka kuwa kulikuwa na kutengeneza mazingira ya
kutaka kumtapeli shamba lake lenye ukubwa mita 63×33 lililoko Kata ya
Kimandolu mtaa wa kijenge juu kata ya kimandolu halmashauri ya jiji la
Arusha.

Bi Angaza amedai katika barua hiyo kuwa chanzo mgogoro huo ni yeye
baada ya kwenda ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuomba msaada wa kutatuliwa
mgogoro kati yake na  Elias Barnabas Chami ambaye alimnyanganya sehemu
shamba na nyumba.

Katika barua hiyo Bi Angasa anadai katika barua hiyo kuwa badala ya
kumsadia kumaliza mgogoro huo alimshawishi amuuzie shamba hilo kwa
milioni 70 ili amuondolee mgogoro huo na kunitaka nimpe akunti namba
ya Benki .

Bi Angaza anadai katika barua hiyo kuwa baada ya kutekeleza agizo
hilo,alielezwa na Gambo kuwa aende Benki ya NBC kusaini hati ya
kupokea milioni 70,hata hivyo anaeleza kuwa baada ya kufika Benki
alielezwa na maafisa wa  Benki hiyo  asaini hati ya kupokea pesa hizo
jambo ambalo alilikataa hadi apewe pesa mkononi.

Anaendelea kudai kuwa baada ya kukataa maofisa wa Benki walimtaka
aondoke,na kumlazimu kurudi kwa Mkuu wa Mkoa Gambo ili amueleze
alichojibiwa na maofisa wa Benki,hata hivyo alipofika kwa Mkuu wa Mkoa
aliambiwa kwa kuwa amekataa kusaini ile karatasi basi hawezi kumsadia
tena.

Katika barua hiyo anamuomba Waziri William Lukuvi amsaidie
kumrejeshelea shamba na nyumba yake,huku akisisitiza kuwa yeye  hana
mtoto wala mtu wa kumsaidia kwa sasa.

Anaeleza kuwa baada ya changamoto hiyo alimfuata mkuu wa wilaya ya
Arusha Gabriel Daqarro katika ofisi yake kutokna na miguu kuuma
alishindwa kupanda juu lakini mkuu huyo wa wilaya pia alishindwa
kumfuata kumsikiliza licha ya kupewa taarifa za uwepo wake.

Alieenda mbali na kutokuwa na imani na uongozi wa mkoa licha ya
kuingia mkuu wa mkoa mpy Idd Kimanta huku akiweka tumaini lake kwa
waziri Lukuvi kuweza kumsaidia kulipatia ufumbuzi suala hilo.

Hata hivyo juhudi mbali mbali zimeendelea kumtafuta aliyekuwa mkuu wa
mkoa wa Arusha Mrisho Gambo lakini hakuweza kupatikana kuzipatia
majibu tuhuma ambazo zimeelekezwa kwake licha ya kupigiwa simu mara
kwa mara bila majibu kwani haipatikani hewani na pia  kutumia ujumbe
mfupi bila majibu.

Juhudi za kumtafuta meneja wa benki ya NBC Tawi la Boma Road iliaweze
kujibu tuhuma hizo zilizoelekezwa kwa benki hiyo simu yake iliita kwa
siku nzima ya jana bila majibu ila juhudi zinaendelea kumtafuta ili
aweze kujibu tuhuma hizo zilizoelekezwa kwake na Bibi Angaza.

Katika hatua Nyingine Kikongwe mwenye umri wa Miaka 94,Ndesinio Ndewario Nko Mkazi wa Kijiji cha Nkoaranga,Wilayani Arumeru ,Mkoani Arusha,amemwomba rais John
Magufuli kumsaidia kupata eneo lake baada ya kushinda kesi mahakamani
lakini uongozi wa wilaya umeshindwa kutekeleza amri ya Mahakama.

Akiongea kwa uchungu na vyombo vya habari ,Ndesinio alisema kuwa
alishitakiana na mtoto wake aitwaye Emmanuel Nko ambaye aliuza
kinyemela eneo hilo lenye ukubwa wa ekari moja lililopo eneo la Kiwawa
wilayani humo.

Alisema katika kesi mbalimbali zilizounguruma kuanzia baraza la Ardhi
la Kata,baraza la wilaya, Mahakama kuu na Mahakama ya Rufaa alishinda
na Mahakama hizo kumtambua yeye kama mmiliki halali wa eneo husika.

Kikongwe huyo alieleza kuwa  kijana wake huyo  aliuza eneo hilo
kinyemela  mwaka 2012 kwa Ester Palangyo (Mama chai Jana) mkazi wa
Maji ya chai wilayani humo bila kuishirikisha familia wakati akijua si
Mali yake nani kinyume cha sheria.

Baada ya kumalizika kwa kesi hiyo ,Mahakama ya rufaa ilitoa maelekezo
kesi hiyo irejeshwe baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ambao
walitekeleza amri ya mahakama ya rufani kwa kukabidhi eneo kwa mdai.

Baraza hilo la Ardhi na Nyumba la wilaya la Arusha lilimwandikia barua
Mkuu wa wilaya ya Arumeru yenye kumbukumbu namba DLHT/MISC.APP.NO.48
ya mwaka 2013 kuitambulisha kampuni ya udalali ya REGIZ COMPANY LTD
kwa ajili ya utekelezaji wa Amri ya baraza katika shauri namba 48/2013
ya mdai Ndesinio Ndewario dhidi ya mdaiwa  Immanuel Ndewario Nko.

Alisema kuwa Kampuni ya udalali ya Regiz kupitia barua yake yenye
kumbukumbu namba RGZ/AR/48/2020 ilitekeleza hukumu ya shauri hilo
namba 48/2013 ikiwa ni pamoja na kuondoa nyumba zilizokuwa zimejengwa
na kumkabidhi mdai mbele ya watendaji wa ofisi ya kata ya Imbaseni.

Bibi huyo alidai kwamba julai 23,2020 alipokea barua kutoka kwa Mkuu
wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro yenye kumbukumbu namba
DC/ARUM/W.10/1XL/62 ya kusitisha kufika katika eneo hilo jambo ambalo
amedai ni ukiukwaji wa amri ya Mahakama na kumtaka rais John Magufuli
kuingilia kati na msaidia kupata eneo lake kwani ofisi ya Mkuu wa
wilaya inajinufaisha kupitia mgogoro huo uliokuwa umemalizwa na
Mahakama.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akiongelea suala
hilo ofisini kwake alisema kuwa ni kweli ofisi yake imesitisha
utekelezaji wa Amri hiyo ya mahakama baada ya kuwepo kwa viashiria ya
uvunjifu wa amani.

Akiongelea suala hilo alisema kuwa hawezi kutekeleza amri ya sasa
inayotoka baraza la Ardhi wakati kuna amri nyingine ya nyuma ya
Mahakama kuu juu ya shauri hilo ambayo ulitolewa na ilikuwa
haijatekelezwa.

“Hapa lazima muelewe kwamba kuna amri mbili zilizotolewa na mimi
naanza kutekeleza amri ya Mahakama ndio maana nimesitisha kwanza amri
ya sasa ya baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya “alisema Murro

Kabla ya kusitisha kwa Amri hiyo Mkuu huyo wa wilaya aliwahi kusaini
hati ya utekelezaji wa Amri ya Baraza Kupitia barua ya kampuni ya
udalali ya REGIZ yenye kumbukumbu namba RGZ/MB/AR/48/2020 iliyosaimiwa
Mei 19 ,Mwaka huu 2020.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana