Bah Ndaw aliyekuwa Waziri wa Ulinzi ameteuliwa kama Rais wa Serikali ya mpito nchini Mali, uteuzi huo umefanywa na Kanali Assimi Goita aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi mwezi Agosti na yeye atakuwa Makamu wa Rais.
Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imekuwa ikiwashiniza Wanajeshi kurudisha madaraka kwa raia baada ya kuondolewa kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Ibrahim Boubacar Keita.
Hata hivyo, bado haijafahamika kama Ndaw atakubaliwa na ECOWAS ambayo wiki iliyopita, ilitishia kuiongezea Mali vikwazo vya kiuchumi Mali, Serikali ya mpito inatarajiwa kuapishwa Septemba 25
.
Post a Comment