Baada ya Fatuma Karume kuondolewa katika orodha ya Mawakili Tanganyika kufuatia Kikao Cha Kamati ya Maadili ya Mawakili kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam, na kumkuta na hatia ya ukiukwaji mkubwa wa maadili, hatua hiyo ikifuatiwa na ile ya Kampuni ya IMMA Advocates, kumfuta rasmi kazi tangu Jumatatu wiki hii akidaiwa kukaidi onyo alilopewa na Mawakili washirika, kadhia zaidi zimeibulika dhidi yake.
Imedaiwa kuwa Fatuma akiwa mfanyakazi wa IMMA Advocates alikuwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo utoro kazini, ukosefu wa nidhamu kwa mawakili washirika, kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, kukosa leseni ya uwakili na kujihusisha na vitendo vya upewaji wa fedha chafu kutoka katika Shirika la Ford Foundation linaloifadhili Taasisi isiyo ya kiserikali ya Change Tanzania iliyo chini ya Maria Sarungi anayesemekana kujihusisha nae mapenzi ya jinsia moja, almaarufu Kusagana.
Shirika hilo la Ford Foundation linadaiwa kufadhili watu na Taasisi mbalimbali Barani Afrika kwajili ya kile kinachoitwa, kuhamasisha Demokrasia na utawala wa sheria huku ikidaiwa kuwa hapa nchini Tanzania wanufaika wa mabilioni ya Shirika hilo ni Didier Mlawa, Ansbert Ngurumo, Maria Sarungi, kupitia Taasisi ya Change Tanzania Taasisi ambayo inadaiwa huwalipa vijana kufanya harakati katika mitandao ya kijamii hususani katika agenda za kuipinga serikali na inadaiwa Vijana kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam ni miongoni mwa wanufaika wakubwa.
Inadaiwa kwamba kwa miaka mingi Fatma Karume amekuwa akijihusisha na mashirika yenye mlengo wa Taasisi hiyo ya Ford Foundation, hivyo kufukuzwa kwake IMMA Advocates ni njia nyingine ambayo itampa fursa mpya ya kuajiriwa katika Taasisi hiyo au mashirika mengine lenye mlengo wa Ford Foundation.
Post a Comment