Na Alodia Babara, Bukoba
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Bukoba mjini wametakiwa kujifuta mavumbi na kumchagua mgombea Ubunge anayetokana na CCM Ili kuleta maendelea katika Manispaa ya Bukoba.
Hayo yalisemwa na mgombea ubunge wa CCM katika jimbo la Bukoba mjini Steven Byabato, katika uzinduzi wa kampeini jimboni humo ambapo alisema, kwa kipindi cha miaka iliyopita wananchi walifanya kosa na kuchagua mbunge wa upinzani jambo ambalo lilisababisha baadhi ya miradi ya maendeleo kukwama ikiwemo ujenzi wa standi.
Byabato ameeleza kuwa, katika kipindi cha miaka mitano wana CCM wa jimbo hilo walipotea sana hivyo wana Bukoba wanyanyuke wajifute mavumbi wachague CCM, waweke mnara ili yawepo mawasiliano kati ya jimbo na Serikali Kuu, maana kwa kipindi cha miaka mitano haukuwepo mnara ndiyo maana jimbo la Bukoba ilishindikana kujengwa soko pamoja na stendi ya mabasi mjini Bukoba.
Alisema jamii ya wanabukoba wana changamoto ya umiliki wa ardhi na kuwa moja ya kipaumbele chake ni kuhakikisha anaweka utaratibu wa kuitatua migogoro ya ardhi Ili iweze kupungua kama siyo kuisha kabisa.
Kwa upande wake mjumbe wa mkutano mkuu Taifa Wirbroad Mtabuzi amesema jamii ya Bukoba isirudie makosa ya mwaka 2015 kwani imekosa maendeleo kwa miaka mitano na kuwa sumu haionjwi wasirudie kosa.
" Wenye mapenzi mema na uchu wa maendeleo tunaowajibu wa kutokubali kugawanyika ushindi ni lazima na ushindi tayari tunao".Amesema Mnec Mtabuzi.
Kwa upande wake mgombea katika kura za maoni wa jimbo hilo aliyekuwa amekuwa wa Kwanza Almasoud Kalumuna amemuombea kura Byabato na kusema familia ya baba yake inawaomba wanabukoba kumpatia kura ili akapeperushe bendera ya chama.
Naye Tobias Mwesiga aliyekuwa mgombea nafasi ya tatu kura za maoni jimbo la Nkenge Wilayani Mesenyi amewaomba wananchi wa jimbo la Bukoba kuchagua chama cha mapinduzi kuanzia ngazi ya Urais, ubunge na udiwani.
Aidha Barozi Hamisi Kagasheki akimnadi mgombea ubunge amesema Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania amewahi kupita Bukoba mara mbili bila kusimama Bukoba mjini kutokana na kutokuwepo kwa mbunge anayetokana na CCM hivyo kama wanabukoba wanataka maendeleo wachague ccm kuanzia Rais wabunge na madiwani.
Post a Comment