Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akipungia mkono alipowasili kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma kwa ajili ya kampeni za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.
CCM Blog, Kigoma
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Rais Dk. John Magufuli leo amefichua siri yake iliyomsukuma kuteua mawaziri watatu kutoka mkoa wa Kigoma, akisema alipoingia madarakani alitengeneza mkakati wa kutosha kwa kuteua mawaziri watatu kutoka mkoa huo na kisha kuwaweka kwenye Wizara nyeti lengo lake kuu likiwa kuuinua mkoa huo ili usiwe nyuma kimaendeleo.
Akizungumza na wananchi mkoani Kigoma, kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Rais Dk. Magufuli amesema miongoni mwa lengo lake la kuteua mawaziri hao ni kuufanya mkoa wa Kigoma kuwa katika ramani ya nchi na hivyo kufunguka na kuwa juu kiuchumi.
Kuhusu zao la Mchikichi, Dk. Magufuli amesema CCM ilipoingia madarakani tena kwa awamu ya tano, mwaka 2015 aliamua kulifufua zao kwa lengo la kuufanya mkoa wa Kigoma kuinuliwa kichumi na zao hilo.
"Nimesikia mtu fulani akisema eti wao ndiyo wamefufua zao la mchikichi, nikimtuma mtu mwingine anasema yeye, mimi nilimtuma Majaliwa (Waziri Mkuu Kassim Majaliwa) kwa lengo la kufufua zao hili, Kigoma nawapend sana, nataka Kigoma ipande juu," alisema Dk. Magufuli.
Post a Comment