Mimi ni mkazi wa Kawe, kwa vile sasa tuko kwenye kampeni za uchaguzi nina maswali ambayo nahitaji nijibiwe ili tumtendee haki huyu Mbunge wetu aliyemaliza muda wake, Ndugu Halima Mdee, ambaye baada ya kuwa Mbunge wa Kawe kwa vipindi viwili mfululizo na sasa anaomba tena tumchague.
Swali lenyewe si kubwa sana ila linahitaji mtu atakayelijibu atumie hekima na busara ili jibu hilo liwe limeshiba na kumridhisha kila Mwana Kawe.
Swali lenyewe ni hili; je, kuna mtu yoyote anaweza kutueleza japo jambo moja tu, ambalo huyu Mheshimiwa wetu Halima Mdee amelifanyia jimbo la Kawe katika kipindi chake chote cha miaka kumi (10) ili tumfanyie assessment kama anastahili kuongezewa miaka mitano mingine, or she did nothing hivyo anastahili apumzishwe?.
Declaration of Interest
Japo mimi ni Kada na Afisa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini andiko hili sio la ukada au propaganda za kampeni za uchaguzi, bali ni andiko hojaji ya halali na swali la ukweli la mwana Kawe, kuuliza Mheshimiwa Halima Mdee ameifanyia nini Kawe in the past 10 years kustahili kuendelea?.
Rais John Kennedy wa Marekani aliwahi kusema, "usijiulize Marekani imekufanyia nini, bali ujiulize wewe utaifanyia nini Marekani". MheshimiwaHalima Mdee ndie Mbunge wetu Kawe kwa kipindi cha miaka 10, naomba kuuliza kwa anayejua, Jee Mheshimiwa Halima Mdee ameifanyia nini Kawe?.
Najua kuna watu watasema kazi ya kuleta maendeleo ni kazi ya serikali, kazi ya Mbunge ni kuisimamia serikali, lakini bila shaka, tumekuwa tukishuhudia wabunge wa majimbo mengine wakipigamia majimbo yao Bungeni, Je? Mbunge wetu Mhesimiwa sana Halima Mdee aliwahi kupigania nini cha maendeleo ya Kawe?. Kama kuna aliyewahi kumsikia au anakijua alichopigania hata kitu kimoja tuu ajitokeze kutueleza.
Si mnajua kuna zile fedha za Mfuko wa Jimbo? Jee kuna mwana Kawe yeyote, aliwahi kumshuhudia Mbunge wetu huyu Mheshimiwa sana Halima Mdee akifika eneo lolote la Kawe na kuchangia shughuli zozote za maendeleo kupitia fedha za mfuko huo wa Jimbo?.
By the way: Nilikuwa mahali nikamsikia Askofu msomi Daktari Gwajima akieleza mambo ambayo kidogo nilishangaa kuyasikia, maana sikuwa nikiyajua, siyo kwa sababu nyingine ila kwa kuwa sikuwa nikimfuatilia kama nilivyokuwa nikimfuatilia Mbunge wetu Mwanadada, Halima Mdee.
Kumbe huyu Askofu ni mdau mkubwa wa maendeleo ya watu wa Kawe kwa kipindi kirefu na ameisha fanya mambo makubwa kwa wana Kawe kama Mwananchi tuu wa kawaida bila hata kujua kuwa kuna siku atakuja kugombea ubunge wa Kawe.
Kumbe Askofu Gwajima baada ya kuhamia Kunduchi Salasala, alikuta kuna tatizo la maji, na kwa kuwa eneo la Kunduchi ni eneo la pembezoni mwa bahari ambako ukichimba visima vifupi unapata maji chumvi, Mtu wa watu Askofu Gwajima kwanza alihakikisha anagharamia kuchimbwa visima virefu 12 vya mita 300 kwenda chini ili kupata maji safi na salama yasiyo na chumvi kwa ajili ya wana Kawe!
Misima hivyo vilinufaisha wengi wakiwemo Waislam ambao kwenye misikiti saba (7) ya Salasala walifikiwa na maji hayo na kuondokana na adha ya uhaba wa maji ya kutawadha kabla ya kuswali.
Kisha akayatafuta maji ya Dawasa (zamani Dawasco) yakawa yanapita mbali, akaamua kuomba kibali Dawasco (ya wakati huo), akanunua mabomba kama yao kusambaza maji, akayatandika kuwatumia mafundi wa Mamlaka hiyo iliyokuwa ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasco), akanunua pampu ya mamilioni ya fedha kutoka Ujerumani, akanunua mita za maji kama za Dawasco na kusambaza maji kwenye kaya 250 za majirani zake wanaomzunguka na sasa wanapata maji safi na salama!.
Askofu Gwajima tayari ameisha saidia magari saba (7) ya kuhudumia wagonjwa yaani Ambulance kwenye hospitali mbalimbali huku akiahidi pia kutoa magari ya wagonjwa kwenye hospitali za Kawe na Kinondoni!.
Gwajima nilimsikia akisema kwamba kazi ya kuwaletea maendeleo Watanzania sio kazi ya serikali pekee, ni kazi ya wananchi kwa kushirikiana na serikali, hivyo hapo alipo, tayari ameagiza tingatinga la kuchonga barabara na malori mawili ya tipper, ambapo barabara zote za Kawe na Kinondoni zitachongwa, vijana wa Kawe watapatiwa ajira za kuchimba mitaro ya maji, serikali itabaki kazi ya kuziwekea tu lami hizo barabara!.
Mwana Kawe yoyote akiyasikia haya aliyoyafanya Kawe Askofu Gwajima kabla hata hajawa Mbunge, ukilinganisha na alichofanya Mheshimiwa wetu Halima Mdee kipindi chake chote cha miaka yake kumi akiambiwa amchague mmoja kati ya hawa wawili, atamchagua nani?.
Je? Hautakubaliana na kwamba umefika wakati tumshukuru Mheshimiwa wetu Halima Mdee kwa utumishi wake wa miaka kumi Kawe na tumuage kwa upendo, heshima na taadhima kwa kumwambia, Bye Bye Mheshimiwa wetu kipenzi, Kisha tumkaribishe Askofu Dk. Josephat Gwajima kwa kumwambia, Karibu Kawe Askofu Gwajima ili uikamilishe kazi nzuri uliyokwishaanza kuitenda kabla hata hujawa Mbunge.
Ewe mwana Kawe usijivunge, kumbuka zama hizi hapendwi mtu yanapendwa maendeleo, mimi kwa upande wangu nasema bila kificho, Askofu Gwajima kama utabahatika kusoma andiko hili nasema kura yangu ni halali kwako, weee chukua! na kila mwana Kawe aweke dhamira hiyo, ikifika siku ya Jumatano ya Oktoba 28, 2020, kura zoooote kwa Gwajima ili CCM itambe kwa ushindi wa kishondo.
Ndimi Bashir Nkoromo, Mkazi Kindakindaki wa Kawe, 0712498008
Post a Comment