Mkuu wa Jeshi La Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema Jeshi la Polisi nchini limeendelea kuimarisha usalama hususani maeneo ya bandari bubu ambazo zimekuwa zikitumika kuingiza bidhaa za magendo na wahamiaji haramu na kukwepa ushuru wa serikali.
IGP Sirro amesema hayo leo wakati alipofanya ziara ya ukaguzi mkoani Pwani ambapo alizitaka idara zote za serikali zilizopo katika bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyojitokeza katika eneo hilo.
Kuhusu Zanzibar, IGP Sirro amesema kuwa, Jeshi la Polisi limeendelea kuimarisha ulinzi na usalama hasa katika kipindi hiki cha kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu na kwamba yeyote atakayejihusisha na uhalifu au uvunjifu wa amani atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani
Post a Comment