Featured

    Featured Posts

IPIGIENI CCM KURA YA MAFIGA MATATU-OKASH



Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia CCM, Halima Okash (kulia), akiwaomba kwa unyenyekevu wanawake na familia zao kuipigia CCM  kura za mafiga matatu ya Urais kwa Dk John Magufuli, wabunge na madiwani katika kikao cha ndani  cha kupanga mikakati ya ushindi kwenye Kata ya Mvumi Makulu
Okash akielezea mambo mazuri yaliyomo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika kikao hicho.


Na Mwandishi Wetu, Mvumi.

MGOMBEA Ubunge Viti Maalumu Mkoa wa  Dodoma kupitia Chama Cha Mapinduzi, Halima Okash amewasihi wanawake kuwa mabalozi kuhakikisha wanazishawishi familia zao kuipigia kura CCM kwa mtindo wa Mafiga Matatu.

Ombi hilo alilitoa wakati wa vikao vya ndani katika Kata ya Mvumi Makulu, mkoani humo, ambapo alifafanua kuwa mafiga matatu ni kumpigia kura Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli, wagombea ubunge na madiwani wa chama hicho.

"Nawaomba wanawake muwe mabalozi wetu huko majumbani mwenu, mhakikishe familia zenu zote  zinapiga kura za mafiga matatu kwa wagombea wa CCM, yaani Rais, wabunge na madiwani ili tupate ushindi wa kishindo," alisema Okash. 


Aidha, Okash katika vikao vya ndani, aliwasisitiza wanawake kudumisha umoja, upendo, mshikamano na amani hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi na kwamba mambo hayo yakivurugika, waathirika wakubwa ni akina mama na watoto.

Okash ambaye ni mmoja wa wapambanaji wakubwa katika kampeni hizi za CCM, amesema haoni sababu ya Dk. Magufuli kutopigiwa kura nyingi, kwani kila mmoja wetu ameona mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi kifupi cha uongozi wake wa Serikali ya Awamu ya Tano.

"Mwenye macho haambiwi tazama, miaka mitatu iliyopita Dodoma haikupiga maendeleo kama ilivyo sasa, uamuzi wa Dk Magufuli kuhamishia Makao Makuu Dodoma, umewanufaisha sana wananchi wa jiji la Dodoma na vitongoji vyake,"alisema Okash.

Okash, alitaja baadhi ya mambo makubwa yaliyofanywa na yanayoendelea kutekelezwa Dodoma chini ya Uongozi wa Dk. Magufuli kuwa ni; Ujenzi wa barabara za kisasa ikiwemo ya Pete (Ring Road) ya njia nne itakayozunguka jiji la Dodoma, ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Hospitali za kisasa ikiwemo ya Benjamin Mkapa, Soko la kisasa la Ndugai, Stendi ya kisasa ya mabasi na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato unaoanza kujengwa hivi karibuni. Pia ameahidi kujenga uwanja mkubwa wa kisasa wa michezo.
 
 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana